Vigingi vitano Rugemalira Kudai Fidia Mahakamani




KUACHIWA huru kwa mfanyabiashara James Rugemarila baada ya kukaa garezani bila kesi kuanza kusikilizwa kwa zaidi ya miaka minne kumezua mjadala huku mawakili wakisema katika mazingira hayo, anaweza kudai fidia kwa madhara aliyopata.

Hata hivyo, wataalamu hao wa sheria wana angalizo kwamba itakuwa ngumu kwa mfanyabiashara huyo kushinda kesi hiyo ya madai ya fidia, wakilinganisha na dhana ya 'ngamia kupenya kwenye tundu la sindano'.

Katika mazungumzo na Nipashe kwa nyakati tofauti mkoani Dar es Salaam, mawakili wa kujitegemea walisema mhusika baada ya kuachiwa huru, anaweza kudai fidia, lakini tayari Mahakama ya Rufani ilishatoa vigezo vitano kwa kuzingatiwa na endapo mhusika atakidhi, anaweza kudai fidia mahakamani.

Wakili Benedict Ishabakaki aliiambia Nipashe kuwa mtu aliyekamatwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma, akafunguliwa mashtaka mahakamani na baada ya kukaa mahabusu kwa muda mrefu kesi inafutwa kwa kukosekana kwa ushahidi anaweza kudai fidia.

"Ukiachiwa na ukawa umepata madhara yoyote, unafungua kesi dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kudai fidia," alisema.


Wakili huyo alirejea uamuzi wa Mahakama ya Rufani katika kesi ya Jeremiah Kamama dhidi ya Bugomola Mayandi, rufani namba 4 ya mwaka 1981, vilipotolewa vigezo vya kudai fidia.

"Ili udai fidia kuna vigezo vitano: Cha kwanza kesi husika lazima iwe imesikilizwa; pili, mhusika awe ameshinda kesi; tatu, mhusika afungue madai ya fidia; nne, kama hakukuwa na sababu inayofaa na inayowezekana kuwapo kwa mashtaka kama hayo; na kigezo cha tano mhusika lazima aoneshe madhara aliyopata, mfano kwa kukaa mahabusu muda mrefu alikosa kazi au madhara mengine aliyopata," alifafanua.

Alipoulizwa kuhusu suala la Rugemarila kama anaweza kukidhi vigezo au la, Wakili huyo alisema mfanyabiashara huyo alifutiwa mashtaka, hivyo ni ngumu kwa vigezo hivyo kushinda kesi ya kudai fidia, lakini anaweza kufungua shauri akadai fidia.


Wakili Majura Magafu akizungumzia suala hilo, alisema DPP anapofuta kesi na kumwachia huru mhusika, aliyeachiwa anayo haki ya kupeleka madai mahakamani ili alipwe fidia kwa madhara aliyoyapata kwa muda wote huo aliokaa mahabusu.

"Mahakama itakapojiridhisha na madai inaweza kuamua alipwe," alisema Wakili Magafu.

Wakili Casto Rweikiza, akifafanua zaidi kuhusu suala hilo, alisema mtuhumiwa anapopelekwa mahakamani mbele ya hakimu na kusomewa mashtaka, upelelezi unatakiwa kufanyika ndani ya siku 60.

Alisema siku hizo zikiisha, mahakama yenyewe kwa kuliona ama kwa washtakiwa kupitia mawakili wao kuwasilisha maombi, mahakama inaweza kuliondoa shauri hilo

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad