Wafahamu Wanyama 10 Wenye Thamani zaidi Duniani





Je! Ni viumbe vipi vilivyo na thamani zaidi kifedha? Yaani wanyama ghali zaidi ulimwenguni, Jibu linaweza kushangazana pia kuweka wazi matukio ya ajabu juu ya vipaumbele na uasilia wa mwanadamu.
Bata
Siku moja, kuna bata alikuwa anapigwa mnada. Na cha kushangaza ni kwamba bata huyo kwa jina la Muscovy Drake aliibuka kuwa maarufu baada ya kushinda tuzo katika maonyesho ya wanyama na muonekano wake wa kuvutia.

"Ana tabia nzuri sana. Yeye ni msafi kila wakati, anajilinda mwenyewe na unapomwonesha kwa watu, anapenda kutazamwa au kupewa kipaumbele", mmiliki wake Graham Hicks aliambia BBC wakati huo.

Lakini mmiliki wake Hicks alikuwa anakaribia kustaafu kutokana na ufugaji, na hapo ndipo alipoamua kumuuza bata wake, pamoja na bata wengine kama vile bata bukini na ndege.

Kukawa na uvumi kwamba wafugaji kutoka nje ya nchi walikuwa wakitafuta kumnunua drake ili kupata mbegu yake.

Mnada ulipoanza, hata hivyo, kulikuwa na matukio ya kushangaza.

Hicks asiyejulikana, Houghton-Wallace alikuwa amekusanya mkutano, ambao walikuwa wameungana pamoja kumnunua bata wake maarufu.

Bata

Zabuni ilianza kwa Pauni 900 ($ 1,250 / € 1,050), lakini bei iliendelea kuongezeka.

Baada ya kuwekwa kwa zabuni ya mwisho, "chumba kilitulia na ilionekana kama zabuni hiyo imefikia kilele chake", anakumbuka.

Baada ya kushinda kwa zabuni ya Pauni 1,500 ($ 2,070 / € 1,760) - jumla ya kiwango kilichofikiwa kikawa ni cha kuvunja rekodi kwa mauzo ya bata huyo.

Siku hiyo, bata huyo alikuwa ghali zaidi ulimwenguni, na kuingia kwenye kundi la wanyama wenye thamani zaidi duniani.

Lakini wakati angeweza kudai kuwa bata huyo ni ghali kama almasi, kuna spishi zingine nyingi ambazo zina thamani kubwa zaidi.

Hata hivyo, ukweli ni kwamba, wanyama daima wamekuwa sehemu ya uchumi wa binadamu, na jinsi watu wanavyothamini wanyama wengine kuliko wengine, inaweza kufafanua ukweli wa kushangaza juu ya ulimwengu tunaoishi. Hasa kwa hilo, ukiangalia bei ambazo watu wamekuwa tayari kulipa kwa ajili ya wanyama wanaowapenda.

Fikiria moja ya viumbe wa shambani wanaopatikana kila mahali.

Kondoo
Kwa makadirio mengine, kunaweza kuwa na kondoo bilioni moja ulimwenguni, na wengi wao hawana thamani sana.

Lakini mahali pengine nchini Uingereza, kuna kondoo wa kipekee anayeitwa 'Double Diamond', ambaye ana thamani ya pesa isiyo ya kawaida. Hana ngozi ya dhahabu. Ni maumbile yake ambayo yanashikilia thamani aliyo nayo.

Yeye ni mfano wa kuvutia sana wa mwana-kondoo wa Texel, uzao ambao asili yake ni kwenye kisiwa kidogo karibu na pwani ya Uholanzi.

Mwisho wa mwaka 2020, ushirika wa wakulima ulimnunua kwa guineas 350,000 - sarafu ya jadi ya minada ya mifugo.

Inapobadilishwa, hiyo ni sawa na £ 367,500 ($ 490,500 / € 411,300).

"Tulilazimika kulipa kiasi hicho cha pesa kupata mbegu hiyo ya kondoo," ushirika huo ulisema na BBC

Kondoo

Lakini kuna ngombe na fahali ambao waliuzwa kwa gharama ya juu zaidi.

Moja ya maarufu waliouzwa kwa gharama ya juu zaidi ni Missy, ngombe wa kike ambaye alinunuliwa kwa $ 1.2m (£ 865,000 / €1m) mnamo mwaka 2009.

Lakini hata yeye amezidiwa na wenzake wa kiume.

Mnamo mwaka wa 2019, fahali wa Angus anayeitwa SAV America 8018 aliuzwa kwa mshauri wa zamani wa utawala wa Trump kwa $ 1.51m (£ 1.1m / € 1.27m).

Sababu ya bei hiyo ya juu?

Thamani kubwa ni shahawa ya fahali huyu, ambayo inaweza kuuzwa.

Bei za wanyama
Lakini kilimo sio uwanja pekee maisha ya mwanadamu huangaika na bei kubwa sana kwasababu ya wanyama.

Watu wengine watalipa pesa nyingi tu kupata wanyama hao.

Nchini Uingereza, bei ya mbwa imepanda wakati wa janga la corona huku baadhi ya wanyama kama mbwa sasa hivi wakiuzwa kwa $ 3,000 ($ 4,160 / € 3,500).

Ikiwa ungejumuisha gharama ya maisha ya kulisha mbwa, pamoja na bili za mifugo na gharama zingine, wamiliki wa wanyama wanalipa makumi ya maelfu.

Mbwa

Lakini rekodi ya kima cha juu kabisa kuwahi kulipwa kwa ajili ya mbwa ni: Yuan milioni 10 ya China, kwa mbwa anayeitwa 'Big Splash'.

Hiyo ni £ 1.1m kwa viwango vya ubadilishaji hela vya leo ($ 1.55m / € 1.3m).

Kizazi cha mbwa huyu kimekuwa kitu cha ishara ya hadhi nchini China katika miaka ya hivi karibuni.

Lakini bei ya juu, iliyolipwa na mfanyabiashara ambaye alitengeneza pesa zake kwa makaa ya mawe, inaweza pia kuwa uwekezaji kwani mbwa ana uwezo wa kuajiriwa kwa wafugaji wengine.

Lakini Je! Vipi kuhusu paka?
Kati ya wanyama wanaofungwa nyumbani ambao bei yao ni ghali ni paka aina ya Savannah, ambaye anaweza kugharimu karibu $ 20,000 kwa mtoto wa paka ni (£ 14,400 / € 16,900).

Kitabu cha rekodi za dunia, Guinness, hakina rekodi ya pesa nyingi zilizolipwa kwa ajili ya kununua paka, na kulingana na ufahamu wa BBC Future, hakuna paka jike wa nyumbani ambaye anakaribia jumla ya mamilioni ya pesa zilizolipwa kwa ajili ya 'Big Splash' - lakini kuna paka ambao wanaweza kumpiku ukiwa utatumia vipimo vingine vya thamani.

Paka

Hata hivyo, kulingana na Kitabu cha rekodi za dunia, Guinness, paka ambaye amewahi kuuuzwa kwa gharama ya juu zaidi alikuwa ni Blackie, ambaye mwaka 1988 aliachiwa urithi wa pauni milioni 7 ($ 9.7m / € 8.2m) baada ya mmiliki wake, muuzaji wa vitu vya kale, kufariki dunia na kuamua kuivunja familia yake.

Thamani ya wanyama wanaoweza kwenda mbio
Hata hivyo, pesa nyingi ambazo zimewahi kutolewa kwa mnyama, angalau kulingana na kitabu cha Guinness, imekuwa kwa wanyama wanaoweza kwenda mbio.

Kwa uzani, mnyama ghali zaidi katika jamii hii atakuwa ndege.

Njiwa ghali zaidi ni New Kim, ambaye aliuzwa kwa mzabuni asiyejulikana nchini China anayejulikana tu kwa jina la uwongo "Super Duper" kwa € 1.6m ($ 1.8m / £ 1.4m) mwishoni mwa mwaka 2020.

Lakini pengine haishangazi kwamba ni farasi wa mashindano ambao wanaongoza kwa bei ya juu.

Kitabu cha Guinness kina mtaja farasi Seattle Dancer kama ghali zaidi, aliyenunuliwa kama mtoto akiwa na miaka 1-2 mnamo mwaka 1985 kwa $ 13.1m (£ 9.4m / € 11m).

Kwa bahati mbaya, farasi Seattle Dancer alipata virusi, na akashindana mara tano tu.

Katika kipindi cha muongo mmoja au miwili iliyopita, wanasayansi wamejaribu kuweka thamani ya kiuchumi kwenye mifumo ya ikolojia kwa kuhesabu "huduma" wanazotoa kwa wanadamu, kuanzia kwa chakula hadi rasilimali wanayotoa kwa faida zaidi ya moja kwa moja, kama vile kusaidia katika kuondokana na kaboni, uchavushaji, burudani na utalii.

Hivi karibuni, Ralph Chami katika Shirika la Fedha Duniani na wenzake walitumia njia ya kuangalia "mnyama mmoja".

Lengo lao likiwa kuhesabu thamani ya ndovu wa msitu wa Kiafrika, na nyangumi mkubwa kutoka pwani ya Amerika Kusini.

Na ikabainika ndovu na nyangumi pia wanasaidia kupunguza kiwango cha dioksidi ya kaboni kwenye anga kupitia miili yao na namna yao ya ulaji.

Ilisemekana kuwa njia kama vile kutumia wanyama hao katika kampeni za mazingira kunaweza kuimarisha thamani yao kwa umma hasa baada ya kuelimishwa juu ya " mchango wao katika kukabiliana na hewa chafuzi kwa mazingira na kushawishi watu kutumia raslimali zao kutunza spishi hizi," Shirika hilo lilisema.

Ni wazi kuwa hakuna jibu rahisi au la moja kwa moja.

"Ukijaribu kuangalia kwa haraka haraka, unaweza kusema pengine bei ya farasi wa mashindano ndio inayoongoza katika orodha hii -lakini kama tulivyochunguza, kuna wanyama wengine wenye thamani kiuchumi au matajiri ambao hawapatikani katika "kununuliwa"

Hata hivyo, kuna mnyama mmoja ambaye bado hatujamtaja, na anayeweza kuwa na thamani ya juu katika bei yake ya kumnunua.

Panda mkubwa
Kwa kweli ni spishi ya mnyama iliyo ghali zaidi, kulingana na kitabu cha Guinness, lakini thamani yake ya kweli inaweza kuwa juu zaidi.

Idadi yao wote inamilikiwa na China, na mbuga nyingi za wanyama - haswa nchini Marekani - lazima zilipe ada ya kukodisha kuwa nao kiasi cha hadi $ 1m kwa mwaka (£ 723,000 / $ 845,000).

Kwa kuwa panda wengi wameishi katika miaka yao ya 20, hiyo inaongeza kiasi kikubwa cha pesa.

Ikiwa watoto watazaliwa, malipo ya mara moja ya hadi $ 600,000 (£ 434,000 / € 507,000) lazima yalipwe pia.

Kwa hiyo, katika orodha ya wanyama wa bei ghali, kuna wale ambao ni muhimu sana - kama vile panda, tembo, nyangumi, mbwa, paka na farasi ambao kwa pamoja thamani yao inaweza kuwa hadi mabilioni ya pesa.

Na kisha kuna bata Drake.

Kwa kweli sio mnyama wa bei ghali sana lakini bado anastahili kupewa nafasi yake.

Kwa mmiliki wake Graham Hicks, hata hivyo, bei ya bata drake labda haikuendana na thamani yake.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad