Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa amewaagiza wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini kuhakikisha wanatenga fedha za mapato ya ndani ili ziweze kutekeleza miradi ya maendeleo itakayotatua kero za wananchi.
Akiongea na Sekretarieti ya Mkoa wa Pwani Leo Waziri Ummy amesema kuwa hatasita kuwachukulia hatua Wakurugenzi watakaoshindwa kutenga fedha za mapato ya ndani kwa ajili ya maendeleo ya wananchi
"Tunakusanya ushuru wa mazao, ushuru kutoka kwa wafanyabishara wadogo, tunawatoza ushuru kupitia huduma, hivyo ni wajibu wetu kurudisha huduma kwa wananchi kwa kutekeleza miradi ya maendeleo amesisitiza Waziri Ummy
Amesema kuwa ni wajibu wa Wakurugenzi kuhakikisha wanatenga fedha za mapato ya ndani kwa ajili ya ujenzi wa miradi ya maendeleo ambayo itatatua kero za wananchi ikiwemo afya, elimu na miundombinu ya barabara
Aidha Amewaagiza Sekretarieti za Mikoa nchini kuhakikisha wanasimamia ukusanyaji wa mapato ya ndani ya Halmashauri na fedha zinazokusanywa zinatengwa kwa ajili ya miradi ya maendeleo