Wakuu wa Mikoa hakikisheni mnawapanga upya Wamachinga - Rais Samia Suluhu




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia  Suluhu Hassan   amewataka  Wakuu wa Mikoa  nchini kuwapanga upya wafanyabiashara ndogondogo maarufu kama machinga bila kutumia nguvu ili wafanye biashara zao kwa kufuata taratibu zilizowekewa .

Amesema hayo  leo  katika hafla ya kuwaapisha viongozi aliowateua  jana tarehe 12 Septemba  katika viwanja vya Ikulu jijini  Dodoma.

“Serikali ilitoa fursa kubwa kwa machinga kufanya biashara za kujipatia kipato kwa uhuru lakini  msitumie fursa  hiyo vibaya na kufanya biashara kiholela ambapo baadhi yao hupanga bidhaa nje ya maduka na kuwazuia wenye maduka kufanya biashara , kitendo ambacho kinakosesha kodi toka kwa wafanyabiashara hao,” alisema Rais Samia.

Aidha, Rais Samia amewataka viongozi aliowapisha na walio katika nafasi mbalimbali za uongozi kutekeleza majukumu yao kikamilifu kwa kuwa mabadiliko aliyofanya katika Baraza la Mawaziri ni yakawaida lakini ni endelevu .

 Vilevile, Rais Samia amewataka watendaji Serikalini  kuendesha shughuli  zao kwa vitendo ili kuwaletea wananchi maendeleo na si kwa maneno makali ambayo hayana tija kwa maendeleo ya wananchi.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad