Wanaume Milioni 1.5 Kutahiriwa Kampeni ya HIV




MRADI wa kuwatahiri wanaume milioni 1.5 wenye umri wa kuanzia miaka 15 hadi 49 uimeanzishwa nchini Sudan Kusini ili kupunguza uwezekano wa kuambukiza virusi vya HIV vinavyosababisha Ukimwi.

 

Utafiti unaonesha kuwa wanaume waliotahiriwa wana hatari ya chini ya kuambukizwa virusi vya HIV kuliko wanaume ambao hawajatahiriwa wanafanya tendo la ngono na mtu wa jinsia tofauti mwenye virusi hivyo.

 

Shirika lisilo la kiserikali la Human Appeal Associates, kwa ushirikiano na wizara ya afya ya nchi hiyo, watawatafuta wanaume watakaojitolea kutahiriwa kwa kipindi cha miaka mitano ijayo. Majimbo matatu pekee kati ya 10 ndio yenye utamaduni wa kutahiri, ndani ya majimbo hayo kutahiri ni mwiko.

 

Serikali imeelezea viwango vya chini vya kutahiri kama hofu kuu ya afya ya umma inapokuja katika suala la kukabiliana na HIV nchini Sudan Kusini.

 

“Viwango vya wanaohitaji kutahiriwa katika mji mkuu Juba pekee ni vya juu sana,” Robert Matthew Uku, kutoka shirika la from Human Appeal Associates, amesema.

Bei Imeshuka! Mnada Mkubwa wa Bajaji Kutikisa Dar Jumamosi Hii – Video

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad