Wapenzi Waliokufa kwa Juisi ya Sumu Wazikwa



Watu wawili waliofariki kwa kunywa sumu katika Kitongoji cha Mlandizi Kata ya Mlandizi Tarafa ya Mlandizi Wilaya ya kipolisi Mlandizi Mkoani Pwani, wamezikwa ijumaa ya Septemba 10, ambapo mwanamke amezikwa Temeke jijini Dar na mwanaume amezikwa Wilaya ya Manga’ka Kijiji cha Napacho mkoani Mtwara.

Watu hao wawili wanaodaiwa kuwa ni Wapenzi, mnamo Septemba 05, walikutwa walifariki katika makazi yao baada ya kunywa kitu kinachodhaniwa ni sumu.

Watu hao ni Godfrey Pius Mandai (48) ambaye alikuwa ni Dereva wa Kampuni na Veronica Gerald ( 42), Mfanyabiashara na mkazi wa Mtwara ambaye alisafiri kutoka Mtwara na kumfuata Mpenzi wake huyo Mlandizi.

“Mwanaume yule alitengeneza juisi ambayo ndani yake ilikuwa na sumu akampa Veronica akanywa na kufariki, Mwanaume alipoona mpenzi wake amefariki na yeye akanywa akafariki…”

“Chanzo ni wivu wa kimapenzi ambapo Mwanaume alikuwa anamtuhumu Veronica kuwa anafanya usaliti, kwenye eneo la tukio tumekuta chupa yenye masalia ya sumu na tumeikuta pia karatasi ambayo inadhaniwa imeandikwa na mmoja wao na imeandikwa ‘HUU NI USALITI TU’” …. alisema Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani , Wankyo Nyigesa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad