Watoto wawili mapacha wamefariki dunia baada ya kuporomoka kutoka ghorofa ya kumi wakati mama yao akijivinjari LIVE katika mtandao wa facebook.
Mapacha hao Moise Petrice wa kiume na Beatrice Petrice pacha wa kike wamekumbwa na umauti huo baada ya kudandia katika dirisha lililokuwa wazi. Tukio hilo limetokea katika jiji la Ploiesti nchini Romania.
Polisi wanasema mama wa watoto hao hakugundua kama wanae wameporomoka na kufariki dunia hadi hapo aliposikia milio ya magari ya kubebea wagonjwa (Ambulance) huku kukiwa na mtu akibisha hodi mlangoni kwake.
Muda wote huo alikuwa LIVE facebook akiongea na wafuasi wanaomfuatilia katika ukurasa wake wa mtandao huo.
Imeelezwa kuwa wakati mama huyo Andreea Violeta Petrice alisahau kufunga dirisha ambalo watoto hao walilitumia kucheza kwa kujaribu kutoka na ndipo walipododondoka na kupoteza maisha.
Baada ya kumfungulia mlango mtu ailyekuwa anabisha hodi alimtaarifu kuwa kulikuwa na watoto mapacha wamedondoka na kufariki.
Mama huyo kwa haraka alikwenda chumbani kwa watoto wake ili kujua kama ni wake na ndipo alipogundua kuwa hawakuwa ndani na dirisha lilikuwa wazi.