Hatimaye baada ya miaka minne, Yanga imeshinda Medali ya kwanza ya maana.. .. Imeshinda Ngao ya Jamii baada ya kuichapa Simba 1-0 siku ya Jumamosi pale kwa Mkapa.. Ni ajabu na kweli.
.
Baada ya ushindi ule, tumaini jipya limemka pale Jangwani.. Mashabiki wa Yanga wameanza kuamini kuwa huenda huu ukawa msimu wa neema kwao.. Pengine wanaweza kushinda taji jingine msimu.. Wataweza kweli?
.
Hata hivyo #amkanagiftmacha inakupa tathmini ya namna ambavyo Yanga inaweza kushinda ubingwa wa Ligi Kuu msimu huu.
.
1. Kushinda mechi za mikoani
Hapa ndipo Yanga inapokwama zaidi kwa sasa.. Yanga imekuwa ikiacha alama nyingi mikoani ambazo mwisho wa msimu huwaondoa katika mbio za ubingwa. Msimu uliopita waliacha pointi Mbeya, Sumbawanga, Tanga, Moshi, Lindi na Mwanza.. Lazima wabadilike katika hili kama wanataka kushinda ubingwa.
.
2. Kupunguza idadi ya sare
Wataalam wanasema ni bora ufungwe mechi moja kuliko kupata sare mbili.. Sare zinaifanya timu ionekane kama bado ipo kwenye ushindani lakini kiuhalisia inapoteza alama zaidi.. Yanga msimu uliopita ilipata sare nyingi kuliko timu yoyote iliyokuwepo ndani ya tano bora.. Lazima wapunguze hili msimu huu.
.
3. Simba ikichelewa kuchanganya..
Kikosi cha Simba kimepungua ubora kidogo msimu huu.. Wapo wachezaji waliochoka, huku pengo la Chama na Miquissone likihitaji muda zaidi ili kuzibwa.. Wachezaji wengi wapya wanahitaji muda kuzoea Ligi.. Kama Simba itachelewa kuchanganya, huo ni mwanya kwa Yanga kufanya vizuri.
.
4. Wachezaji wenye uzoefu mkubwa
Yanga msimu huu ina wachezaji wengi wenye uzoefu mkubwa.. Mbali na uzoefu, wana uwezo mkubwa pia.. Mfano Khalid Aucho, Yannick Bangala, Fiston Mayele, Djuma Shaban na wengineo.. Wachezaji hawa wanaweza kuibeba Yanga katika nyakati zote.. Ni benchi la ufundi kutazama namna ya kuwatumia.
.
5.Nguvu ya nje ya Uwanja
Kama Yanga imejifunza kwa ilipokwama nje ya uwanja msimu uliopita, basi mambo yatakuwa tofauti msimu huu.. Kuna changamoto kadhaa za kiutawala ziliikwamisha Yanga mwaka jana, ambazo kama zimefanyiwa kazi msimu huu huenda wakaimarika zaidi. Kama viongozi wa Yanga watakosa ushirikiano, hali itakuwa ngumu.
By Gift Macha