YANGA wamefanya uamuzi mgumu. Wameamua kumrejesha kwenye benchi la ufundi la klabu hiyo Kocha Mrundi, Cedrick Kaze
Habari za awali ambazo Mwanaspoti imejiridhisha nazo ni kwamba anakuja kuwa msaidizi wa Nasreddine Nabi ambaye awali alikuwa na mtihani wa kushinda mechi dhidi ya Rivers ugenini na ile ya Simba Jumamosi kulinda kibarua chake
Mbali na Kaze pia inatajwa Yanga wako kwenye mazungumzo na Mwinyi Zahera ambaye yeye anaweza kupewa pia nafasi hiyo au Ukurugenzi wa Ufundi aisuke Yangu Idara zote