Rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma ameshutumu mahakama kwa kutoamini ripoti ya kitabibu na madaktari wa jeshi na amekataa kufanyiwa uchunguzi na daktari aliyechaguliwa na mamlaka ya mashtaka.
Madaktari waliwasilisha ripoti ya siri juu ya afya ya Bwana Zuma kama anamudu kuhudhuria kesi yake.
Msemaji wa mfuko wa Bw Zuma Mzwanele Manyi aliiambia runinga ya ENCA rais huyo wa zamani amechoka afya yake kutiliwa shaka.
Madaktari wa jeshi wanawajibika kwa afya ya marais wote wa zamani.
Bwana Zuma alilazwa hospitalini siku chache baada ya kukamatwa na kufanyiwa upasuaji tarehe 14 mwezi Agosti.
Hivi sasa anatumikia kifungo cha miezi 15 kwa kosa la kudharau mahakama na alitakiwa kuanza kusikiliza kesi yake ya ufisadi.