Mahakama ya juu zaidi imeamuru kuwa rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma ameshindwa katika azma yake ya kubadilisha hukumu ya miezi 15 jela.
Mwezi Julai, Bw Zuma, aliiomba mahakama ya katiba kuondoa hukumu yake, akidai kuwa ilikuwa kali kupita kiasi na kwamba gereza litahatarisha afya na maisha yake.
Bw Zuma alifungwa jela kwa kushindwa kutoa ushahidi katika uchunguzi kuhusu ufisadi dhidi yake. Anakana kufanya kosa lolote.
Amelazwa hospitalini ambako anaendelea kupokea tiba ya ugonjwa ambao haujafichuliwa, na atatumikia kipindi kilichobaki cha hukumu ya miezi 15 nyumbani.