Katibu Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo, Ado Shaibu ameweka wazi kwamba kitendo cha aliyekuwa Mgombea Urais wa chama chao, ndg, Bernad Kamilius Membe kujitokeza hadharani na kudai hakuwahi kuhama CCM ni funzo kwao.
Shaibu ameyaweka wazi hayo leo wakati akifanya mahojiano na wanahabari, ambapo amesema kuwa funzo kubwa la Membe ni Wanasiasa kuheshimiana wakati wa migogoro ya ndani.
Shaibu amefafanua kwamba, Membe hakuwahi kukubaliana na msimamo wa chama kumuunga mkono ndg, Tundu Lissu wa CHADEMA na ilipelekea yeye kuondoka ndani ya chama chao baada ya Uchaguzi Mkuu wa 2020.
Aidha Katibu Mkuu, Shaibu amesisitiza kwamba mpaka sasa wanamheshimu Membe, licha ya kuondoka kwa kuwa hajawakosea heshima kama chama kwa kudhihaki, kuwabeza, au kuwafitisha.
“Sisi tunamtakia kila la kheri kwenye uwanja huu wa siasa. Kuja na kuondoka au kuhama vyama sio jambo jipya katika siasa za Tanzania”, Shaibu.