"Sio sawa kwa viongozi wa Serikali kuingilia mchezo wa soka na kutoa ahadi kwa timu zingine na kusababisha Simba SC inakamiwa na Wachezaji wetu kuumizwa, Timu hazina viwango ila zinakamia sana, ila kwa nini iwe kwa Simba tu (kukamiwa), Ahadi zinazotolewa kuongeza motisha zinaharibu mpira hazina maana yoyote, kama huna uwezo huna tu, Kwa nini ahadi zitolewe wanapokutana na Simba tu?! Zinavuruga mpira"
Mshauri wa bodi ya wakurugenzi Simba SC.
Crescentius Magori