Young Thug Aiharibu Rolls-Royce ya Tsh Mil 600





Rapa maarufu wa pande za Joe Biden namaanisha Marekani, Jeffery Lamar Williams almaarufu kama Young Thug anayetamba na albamu yake ya PRUNK , ameonesha jeuri ya fedha kwa kuiharibu gari yake aina ya Rolls-Royce yenye thamani ya dola za Kimarekani 300,000  ambazo ni zaidi ya shilingi milioni 600 za Kibongo.



Taarifa kutoka kwa watu wa karibu wa staa huyo, zimeeleza kuwa Young Thug aliiharibu gari hiyo kwa lengo la kuitangaza albamu yake mpya ya PRUNK.

 

Katika video inayosambaa mitandaoni, inamuonesha Young Thug akiwa juu ya gari hiyo huku akiwa ameshikilia rungu la mbao na kupiga hadi kuvunja kioo cha mbele cha gari hiyo. Pia katika kipande cha video hiyo fupi wanaonekana marafiki wa karibu  wa Young Thug na viongozi wake wakishiriki kwa pamoja kuiharibu gari hiyo ya thamani!



Gari hiyo iliandikwa jina la albamu yake ya PRUNK ambayo ameiachia wiki iliyopita Oktoba 15, 2021 ambayo ndani yake amewashirikisha mastaa kibao wakiwemo J. Cole, Travis Scott, T.Shyne, Nate Ruess na wengineo.

Na Bakari Mahundu, Dar

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad