Ali Kiba Akataa Kuitwa Jina la Mnyama Yoyote "Mi ni King Naweza Kuwafunga Hao Wanyama Wote"


King Kiba Ama Mfalme Wa Bongo Fleva Kama Anavyoitwa Na Wadau Wa Muziki Ameonekana Kukataa Kuitwa Jina La Mnyama Yoyote Kama Wasanii Wengine Ambavyo Wamekua Wakitumia Majina Ya Wanyama Kama A.K.A Zao, Kiba Amefunguka Kwa Kusema Amelipokea Jina La Mfalme Na Mfalme Anaweza Kuwafuga Wanyama Kwenye Ngome Yake


Kupitia Podcast Ya Swahili Radio Na Mtangazaji Lil Ommy Ameeleza Kuwa Yeye Sio Tembo Wala Mnyama Yoyote, Yeye Ni Alikiba Na Amepewa Jina La King Na Kulipokea Basi Ikumbukwe Kwamba Mfalme Anaweza Kuwafuga Wanyama


Miaka Michache Nyuma @officialalikiba Amewahi Kuhusishwa Na Jina La Tembo Ambalo Kwa Sasa Linatumiwa Na Konde Boy @harmonize_tz , Ikiwa Mpaka Sasa Kuna Wasanii Kadhaa Kama SIMBA(@diamondplatnumz), MBUZI(@younglunya), CHUI(@rayvanny), MAMBA(@dudubaya_mamba_oilchafu), NYATI(@ibraah_tz) Wasanii Hao Na Kadhalika Wamekua Wakitumia Majina Ya Wanyama Kama A.K.A Zao


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad