Amber Lulu Arudi Kwenye Akili yake "Mambo ya Kukaa Uchi ni Ushamba Mimi Nimejilaumu Sana Kwa Picha Nilizokuwa Napiga"


MUUZA nyago (video queen) maarufu ambaye pia ni msanii anayefanya vizuri kwenye anga la Bongo Fleva, Lulu Euggen almaarufu Amber Lulu anasema kuwa, kipindi cha kukaa uchi ili mtu apate umaarufu kimepitwa na wakati badala yake sasa hivi ni mwendo wa kupiga kazi ili maisha yaendelee.

Akizungumza na Gazeti la IJUMAA, Amber Lulu anasema kuwa, kwa upande mwingine hata yeye alikuwa akifanya makosa kuacha mwili wake wazi, lakini sasa akili imemkaa sawa na ana mtoto anayemtegemea kwa kila kitu, hivyo hataki kusikia mambo hayo tena kwenye maisha yake.

“Kukaa uchi na kujiachia wazi sehemu kubwa ya mwili kwa sasa ni ushamba na vitu hivyo vimepitwa na wakati kwa sababu hata mimi ninajilaumu sana kwa nini nilifanya hivyo,” anasema Amber Lulu ambaye ni mama wa mtoto mmoja wa kike aitwaye Arianna.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad