Dar es Salaam. Licha ya umuhimu wake kwa uchumi wa Jiji la Dar es Salaam, mikoa jirani na Taifa kwa ujumla, Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala Barabara (Tanroads), Rogatus Mativila amesema wanashindwa kumalizia kujenga kipande cha kutoka Kimara hadi Kibaha na barabara za kuiunganisha barabara hiyo ya Morogoro na Kituo cha Mabasi cha Magufuli kutokana na ukosefu wa fedha.
“Kimsingi bado ujenzi unaendelea na hatuwezi kutoa mapipa yaliyopo kwenye Barabara ya Morogoro haraka, kwani itapunguza usalama hivyo kuongezeka ajali,” alisema Mativila.
Alisema wameomba fedha ili kukamilisha sehemu hizo na kuondoa baadhi ya changamoto ambazo zimekuwa zikijitokeza kwa watumiaji wa barabara hiyo.
Katika barabara hiyo inayoendelea kujengwa ikiwa na njia nne za kwenda na nne za kurudi, Tanroads wameweka zaidi ya mapipa 4,280 na kingo 274 za zege kutenganisha mpaka na sehemu ya katikati ambayo ni kwa ajili ya Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka (BRT).
“Tumeomba fedha za nyongeza serikalini ili kutengeneza kwa lami kipande cha barabara kutoka stendi na barabara kuu ili kuondoa changamoto ya matope pindi mvua inaponyesha,” alisema Mativila.
Mkurugenzi huyo aliongeza kuwa fedha nyingine zitatumika kujenga mawe ya pembeni mwa Barabara ya Morogoro ili kutengeneza mipaka ya barabara hiyo na eneo linaloachwa kwa matumizi mengine.
“Kwa sasa gapestone (kingo) tulizoweka katikati hatuwezi kutoa, kwani tukifanya hivyo tunaweza kusababisha ajali nyingi, kwani madereva wengi wataendesha magari kwa kasi kutokana na uwazi kuwa mkubwa,” alisema.
Alipotafutwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa kujua kiasi cha fedha zilizoombwa na Tanroads, simu yake iliita kwa muda mrefu bila kupokelewa lakini baada ya kutumiwa ujumbe mfupi wa maneno, alijibu:
“Mimi ndiyo ninafanya mambo mengi. Tutaiweka kwenye utaratibu ili iende vizuri”.
Stendi ya Magufuli
Kwa upande mwingine, uongozi wa Manispaa ya Ubungo umetoa ufafanuzi kuwa changamoto zinazokwamisha kukamilika kwa ujenzi wa baadhi ya maeneo ya Stendi ya Magufuli iliyopo Mbezi Luis ni kutotolewa kwa fedha zinazohitajika kwa wakati.
Ujenzi wa stendi hiyo kwa ajili ya mabasi yaendayo mikoani ulioanza Februari 2019 bado haujakamilika kwa asilimia 100, jambo linalosababisha usumbufu kwa magari yanayosimama wakati wa kupakia na kushusha hasa usiku na asubuhi.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mhandisi wa Manispaa ya Ubungo, Masodoya John ambaye ni msimamizi wa mradi wa ujenzi wa stendi hiyo inayojengwa na kampuni ya Hainan ya China, alisema wanategemea mapato ya ndani kuendeleza ujenzi huo.
“Nikiri malipo huwa yanachelewa lakini sio kwa muda mrefu sana kiasi cha kuathiri utendajikazi kwa sababu ndani ya siku 18 mkandarasi anatakiwa awe ameshalipwa. Kukiwa na mapungufu kwenye kuwasilisha nyaraka ikaonekana kuna sehemu inatakiwa ufafanuzi kwa mwajiri ambaye ni mkurugenzi mtendaji wa manispaa, fedha zinachelewa kutoka,” alisema.
Mtaalamu huyo wa ujenzi alifafanua: “Unaweza kukuta hazijaja tarehe 10 kwa sababu ya mapungufu katika kuandaa nyaraka za malipo.”
John alibainisha changamoto nyingine zinazochelewesha kukamilika kwa ujenzi wa mradi huo kuwa ni kufanya usanifu wa mara kwa mara.
“Kitendo cha magari kulala eneo lile kunaweka ugumu. Kuna wakati tunalazimika kuruhusu magari kutoka na kuingia na changamoto hiyo inamlazimu mkandarasi kusimamisha ujenzi wakati mwingine. Hili linasababishwa na kulitumia eneo kabla ya ujenzi haujaisha,” alisema John.
Mhandisi huyo alisema mkandarasi wa mradi huo anajitahidi kutekeleza kila hatua kulingana na mkataba unavyotaka ambao unadumu hadi Desemba mwaka huu atakapomaliza ujenzi na kukabidhi mradi.
“Mategemeo yetu Desemba tunakabidhiwa mradi wetu ukiwa tayari ili tuanze kulitumia eneo kulingana na malengo yaliyokusudiwa,” alisema John, anayeamini baada ya kukamilika kwa ujenzi huo changamoto hizo zitaisha kwa asilimia kubwa, kwa sasa sehemu iliyokamilika yanasimama mabasi 104. Stendi hiyo ina sehemu ya Barabara ya njia nane Dar-Kibaha yakwama
mwananchi.co.tz
1h
Dar es Salaam. Licha ya umuhimu wake kwa uchumi wa Jiji la Dar es Salaam, mikoa jirani na Taifa kwa ujumla, Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala Barabara (Tanroads), Rogatus Mativila amesema wanashindwa kumalizia kujenga kipande cha kutoka Kimara hadi Kibaha na barabara za kuiunganisha barabara hiyo ya Morogoro na Kituo cha Mabasi cha Magufuli kutokana na ukosefu wa fedha.
“Kimsingi bado ujenzi unaendelea na hatuwezi kutoa mapipa yaliyopo kwenye Barabara ya Morogoro haraka, kwani itapunguza usalama hivyo kuongezeka ajali,” alisema Mativila.
Alisema wameomba fedha ili kukamilisha sehemu hizo na kuondoa baadhi ya changamoto ambazo zimekuwa zikijitokeza kwa watumiaji wa barabara hiyo.
Katika barabara hiyo inayoendelea kujengwa ikiwa na njia nne za kwenda na nne za kurudi, Tanroads wameweka zaidi ya mapipa 4,280 na kingo 274 za zege kutenganisha mpaka na sehemu ya katikati ambayo ni kwa ajili ya Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka (BRT).
“Tumeomba fedha za nyongeza serikalini ili kutengeneza kwa lami kipande cha barabara kutoka stendi na barabara kuu ili kuondoa changamoto ya matope pindi mvua inaponyesha,” alisema Mativila.
Mkurugenzi huyo aliongeza kuwa fedha nyingine zitatumika kujenga mawe ya pembeni mwa Barabara ya Morogoro ili kutengeneza mipaka ya barabara hiyo na eneo linaloachwa kwa matumizi mengine.
“Kwa sasa gapestone (kingo) tulizoweka katikati hatuwezi kutoa, kwani tukifanya hivyo tunaweza kusababisha ajali nyingi, kwani madereva wengi wataendesha magari kwa kasi kutokana na uwazi kuwa mkubwa,” alisema.
Alipotafutwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa kujua kiasi cha fedha zilizoombwa na Tanroads, simu yake iliita kwa muda mrefu bila kupokelewa lakini baada ya kutumiwa ujumbe mfupi wa maneno, alijibu:
“Mimi ndiyo ninafanya mambo mengi. Tutaiweka kwenye utaratibu ili iende vizuri”.
Stendi ya Magufuli
Kwa upande mwingine, uongozi wa Manispaa ya Ubungo umetoa ufafanuzi kuwa changamoto zinazokwamisha kukamilika kwa ujenzi wa baadhi ya maeneo ya Stendi ya Magufuli iliyopo Mbezi Luis ni kutotolewa kwa fedha zinazohitajika kwa wakati.
Ujenzi wa stendi hiyo kwa ajili ya mabasi yaendayo mikoani ulioanza Februari 2019 bado haujakamilika kwa asilimia 100, jambo linalosababisha usumbufu kwa magari yanayosimama wakati wa kupakia na kushusha hasa usiku na asubuhi.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mhandisi wa Manispaa ya Ubungo, Masodoya John ambaye ni msimamizi wa mradi wa ujenzi wa stendi hiyo inayojengwa na kampuni ya Hainan ya China, alisema wanategemea mapato ya ndani kuendeleza ujenzi huo.
“Nikiri malipo huwa yanachelewa lakini sio kwa muda mrefu sana kiasi cha kuathiri utendajikazi kwa sababu ndani ya siku 18 mkandarasi anatakiwa awe ameshalipwa. Kukiwa na mapungufu kwenye kuwasilisha nyaraka ikaonekana kuna sehemu inatakiwa ufafanuzi kwa mwajiri ambaye ni mkurugenzi mtendaji wa manispaa, fedha zinachelewa kutoka,” alisema.
Mtaalamu huyo wa ujenzi alifafanua: “Unaweza kukuta hazijaja tarehe 10 kwa sababu ya mapungufu katika kuandaa nyaraka za malipo.”
John alibainisha changamoto nyingine zinazochelewesha kukamilika kwa ujenzi wa mradi huo kuwa ni kufanya usanifu wa mara kwa mara.
“Kitendo cha magari kulala eneo lile kunaweka ugumu. Kuna wakati tunalazimika kuruhusu magari kutoka na kuingia na changamoto hiyo inamlazimu mkandarasi kusimamisha ujenzi wakati mwingine. Hili linasababishwa na kulitumia eneo kabla ya ujenzi haujaisha,” alisema John.
Mhandisi huyo alisema mkandarasi wa mradi huo anajitahidi kutekeleza kila hatua kulingana na mkataba unavyotaka ambao unadumu hadi Desemba mwaka huu atakapomaliza ujenzi na kukabidhi mradi.
“Mategemeo yetu Desemba tunakabidhiwa mradi wetu ukiwa tayari ili tuanze kulitumia eneo kulingana na malengo yaliyokusudiwa,” alisema John, anayeamini baada ya kukamilika kwa ujenzi huo changamoto hizo zitaisha kwa asilimia kubwa, kwa sasa sehemu iliyokamilika yanasimama mabasi 104. Stendi hiyo ina sehemu ya kuegesha mabasi 204 kwa wakati mmoja, hivyo kukamilika kwake kutawanufaisha wananchi wanaoelekea maeneo tofauti kupitia Barabara ya Morogoro.
John alisema ujenzi wa stendi hiyo yenye thamani ya Sh50.9 bilioni bado unaendelea na kwa sasa mkandarasi anajenga daraja sehemu ambako mabasi yanaingilia. mabasi 204 kwa wakati mmoja, hivyo kukamilika kwake kutawanufaisha wananchi wanaoelekea maeneo tofauti kupitia Barabara ya Morogoro.
John alisema ujenzi wa stendi hiyo yenye thamani ya Sh50.9 bilioni bado unaendelea na kwa sasa mkandarasi anajenga daraja sehemu ambako mabasi yanaingilia.
Mwananchi