Beki Simba "Kumuona Chama kwa Sakho ni Uongo"





BEKI mkongwe na mwenye heshima kwenye soka la Tanzania, Boniphace Pawasa amebainisha kuwa ikiwa mashabiki wa Simba watategemea kuona uwezo wa Clatous Chama kwenye miguu ya Pape Sakho itakuwa ni kudanganyana kwa kuwa inahitaji muda.


Sakho, raia wa Senegal, ni ingizo jipya ndani ya Simba na amekabidhiwa jezi ya Clatous Chama aliyekuwa anavaa namba 17 alipokuwa Simba na msimu uliopita wa 2020/21 alifunga mabao 8 na kutoa pasi 15 za mabao.


Akizungumza na Championi Jumatano, Pawasa alisema kuwa ni lazima kuwe na subira kwa wachezaji wapya wa Simba waliosajiliwa kuweza kuonyesha walichonacho kwenye miguu yao ila ikiwa ni kwa uhitaji wa haraka itakuwa ni kudanganyana.


“Ni suala la muda tu kwa wachezaji wa Simba kuweza kwenda sawa na kuona namna ambavyo muunganiko utakuwa pia na falsafa ya mfumo inayotumika na Kocha Mkuu Didier Gomes ni muhimu ili kuona namna gani Sakho anaweza kuwa kwenye miguu ya Chama ila kwa muda huu tukitaka iwe hivyo tunadanganyana.


“Kwenye miguu yao tunahitaji kuwapa muda ili waweze kuonyesha kile ambacho wanacho, unaona kwamba yupo yule Kanoute (Sadio) ni mchezaji ambaye anafundishika na ana kitu ila ni lazima apewe muda.


“Sakho viwanja itakuwa tatizo kwake hasa kwa soka letu la Afrika pia kwa sasa kuna presha kubwa kutoka kwa wanachama ukizingatia kwamba walikuwa sehemu nzuri baada ya kutinga hatua ya robo fainali Ligi ya Mabingwa kwa sasa wanategemea kufika mbali lakini tukubali tumeingia kwenye biashara ya mpira ipo hivyo Madrid walimchukua Hazard (Eden) katika ubora ila hakuweza kufanya vizuri,” alisema Pawasa.

Lunyamadzo Mlyuka, Dar es Salaam

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad