Rais wa Marekani Joe Biden na Xi Jinping wa China wanatarajiwa kufanya mkutano kabla ya mwisho wa mwaka wakati wasiwasi ukizidi kuongezeka kati ya mataifa hayo mawili yenye nguvu ulimwenguni. Ikulu ya Marekani, White House imesema mkutano huo utafanyika kwa njia ya mtandao.
Hatua hii inafuatia mkutano kati ya mshauri wa masuala ya usalama wa taifa katika ikulu ya White House Jake Sullivan na mshauri wa ngazi za juu wa sera za kigeni wa China Yang Jiechi mjini Zurich.
Profesa wa siasa katika chuo kikuu cha East China Normal Josef Gregory hata hivyo amesema ni mapema mno kuamini mahusiano baina ya mataifa hayo sasa yanaimarika.
Mkutano huo unafuatia mwito wa mwezi uliopita kati ya Biden na Xi ambapo Biden alisisitizia umuhimu wa kuwepo kwa mazingira sawa ya ushindani baina yao.