Breaking News : Lengai Ole Sabaya ahukumiwa miaka 30



Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya leo amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la unyang’anyi wa kutumia silaha


Sabaya na wenzake leo mahakamani
Hukumu yakesi ya unyang’anyi wa kutumia silaha iliyokuwa ikimkabili Sabayahiyo imesomwa leo Ijumaa Oktoba 15, 2021 na Hakimu Mkazi Mwandamizi Odira Amworo.

Kabla ya kuanza kusomwa hukumu, Wakili wa Serikali, Felix Kwetukia aliweka wazi kuwa Jamhuri ipo tayari kupokea hukumu huku upande wa utetezi ukiongozwa na Wakili Moses Mahuna, Silvester Kahunduka na Wakili Fridolin Germelo nao walisema wapo tayari kusikiliza hukumu hiyo.

Hakimu Omworo amesema kuwa imethibitika mshitakiwa wa kwanza alikuwa na bastola ndani na nje kulikuwa na watu wawili wenye silaha hivyo, hakuna shaka duka la shahidi wa kwanza lilivamiwa na watu wenye silaha na lilikuwa chini ya watu wenye silaha.

Washtakiwa, Sabaya na wenzake walifikishwa mahakamani leo saa 3:05 asubuhi, kwa ajili ya hukumu ambapo Oktoba 1 2021 Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Amalia Mushi aliahirisha hukumu hiyo kwa maelezo ya kutokamilisha kuandika hukumu hiyo.

Sabaya alifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Juni 4, mwaka huu baada ya kukamatwa Mei 27 wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad