Shughuli za kuzima moto Mlima Kwaraa wilayani Babati mkoani Manyara bado zinaendelea mpaka sasa ikiwa ni siku ya pili toka moto huo ulipozuka siku ya alhamisi jioni.
Ukiondoa Mlima Hanang uliopo wilayani Hanang, Mlima Kwaraa ndiyo mlima unaofuata kwa urefu mkoani Manyara.
Mlima huo ni moja ya vivutio vikubwa vya watalii wilayani hapa, na mpaka kufikia sasa ofisi ya Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) wilayani Babati inasisistiza wananchi kujitokeza kuuzima moto huo.
Kiongozi mmoja kutoka ofisi ya wakala wa Misitu wilayani Babati aliejitambulisha kwa jina moja Izungo, amesema walipata taarija jana alhamisi saa kumi jioni kutoka kwa wakazi wa kijiji cha Mutuka ambapo ndipo moto ulipoanzia, ambapo viongozi walifika katika eneo hilo na ilipofika usiku walisitisha zoezi hilo.
Miale ya moto na moshi imekuwa ikionekana kutoka mji wa Babati umbali wa Zaidi ya kilomita kumi kutoka eneo la mlima kulikotokea tukio hilo.
Mpaka sasa chanzo cha Moto huo bado hakijafahamika.