Chama cha Demokrasia na Maendeleo, kimesema hakijaridhika na uamuzi uliotolewa na Jaji Kiongozi Mustapha Siyani katika kesi ndogo ndani ya kesi ya msingi inayomkabili Mwenyekiti wao Freeman Mbowe pamoja na wenzake watatu.
Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa CHADEMA John Mnyika, ambapo ameeleza kwamba kama Chama wanatafakari hatua za kuchukua ili haki itendeke dhidi ya Kiongozi wao.
Mnyika ameeleza hayo mudfupi baada ya uamuzi wa mapingamizi mawili yaliyotolewa na Jaji Siyani kwa kueleza kwamba mapingamizi ya maelezo kuchukuliwa baada ya masaa manne kupita na pasipo hiyari ya mshtakiwa.
Katika maamuzi yake amesema kwamba mapingamizi hayo yamekosa mashiko, na kwamba maelezo yalichukuliwa ndani ya masaa manne, na pia maelezo yalitolewa na mshtakiwa wa pili kwa ridhaa yake.
BY: Fatuma Muna