April 14 mwaka 2020 habari ambayo ilitake over kwenye social Media kibongo bongo ni pamoja na hii ya wasanii tokea Kings Music, @officialcheed na @officialikilly_tz kuondoka kwenye Label hiyo huku sababu hasa wakishindwa kutaja ni zipi. Na baadae wakaibukia Konde Gang. Inaaminika Diva the Bawase ndiye aliyekuwa nyuma ya Mchezo baada ya kugombana na Alikiba na akawaconnect Konde Gang maana wakati huo alikuwa anaiva na Harmonize.
Imekaa hivyo kwa muda mrefu, hasa hii leo october 01, Cheed akiwa kwenye Empire ya EFM amedai wakati wanaondoka Kings wala hawakuwa na direction kuwa wanenda wapi na wala @harmonize hahusiki kuwafanya wao waondoke Kings. Walionana na Harmonize baada ya wao kuwa washaondoka muda tu pale Kings.
Wasanii hao washarudi kwenye game huku Cheed akirudi September 29 na goma la Wandia ambalo liko YouTube kwa sasa.
🙏