“Awa mateso kwa familia yake” ndivyo inavyoishia, ilianza hivi “Kijana wa miaka 17 auza figo yake ili kununua iPhone…” Baada ya miaka nane figo iliyobaki ikashindwa kufanya kazi , na yeye kugeuka kuwa mateso kwa familia yake.
Achana na huyo kijana wa China huko ,turudi kwetu Bongo . 2018 ilivuja bi dada mmoja hivi schoolmate akim’force’ Mwana wa Makumbusho pale aliyekuwa classmate wake “ale mchongo kwa haifoni”😄😄
Hujaelewa nini hapo? Mwana alivujisha meseji group la darasa bi dada akiomba “aliwe jicho moja apate macho matatu” kama memes zinavyo sema. Inasikitisha sana.
Ushauri wangu kwa Vijana wenye matumaini angavu mstifute ufahari kwa watu jiepusheni na tamaa tamaa ni chanzo cha mateso na aibu.
Nilikutana na nukuu hii kwenye jarida la maisha jinsi tuyajuavyo imenipa funzo kubwa inasema hivi
“Kununua vitu vya bei ghali kwa mkopo ili kujihisi na kuonekana kuwa tajiri ni kama tu kutumia dawa za kulevya ili ujihisi vizuri”