Daktari Feki Akamatwa Tandahimba





Daktari mmoja aliyejulikana kwa jina la Karim Bakari kutoka kijiji cha Maheha wilaya ya Tandahimba mkoani Mtwara anashikiliwa na jeshi la polisi wilayani humo  kwa kosa la kutoa  huduma za upasuaji na matibabu kwa wagonjwa nyumbani  kwake kinyume na taratibu.


Daktari huyo ambaye alifukuzwa kazi mwaka jana katika hospitali ya wilaya ya Newala kwa tuhuma za kusababisha kifo cha mgongwa aliyefanyiwa upasuaji amesema aliamua kufanya hivyo kutokana na msongo wa mawazo aliokuwa nao na kuomba serikali imsamehe.



Amesema anajua kwamba amefanya kosa kubwa la kisheria la kutoa huduma nyumbani kwake na kuhatarisha maisha ya wananchi anaowapatia huduma jambo ambalo ni hatari 



Mkuu wa wilaya ya Tandahimba Kanali Patrick Sawala amesema kukamatwa kwa daktari huyo ni kutokana na uchunguzi uliofanywa kwa muda mrefu baada ya kupata taarifa kutoka kwa wananchi.



Kanali  Sawala ameliagiza sheji la Polisi wilayani humo kufuata hatua za kisheria na kufuatilia kwa kina wapi ambako alikuwa akipata dawa na vifaa tiba ambavyo vilikuwa vinatumika wakati anatoa huduma nyumbani kwake huki akionya wale wanaoendelea kufanya hivyo katika wilaya yake kuacha mara moja.



Kwa upande wake kaimu mganga mkuu wa wilaya ya Tandahimba Daktari Silas Sembiko amewataka wananchi kuacha tabia ya kupata huduma za afya vichochoroni kwani ni hatari kwa afya zao.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad