Mkuu wa Wilaya ya Lushoto Mkoani Tanga Kalisti Lazaro ameahidi kuchukua hatua kali za kisheria kwa Watumishi watakaobain goika kushiriki kubadili matumizi ya fedha za zahanati ya Mziragembei na kuzipeleka kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa uliopita.
Hayo aliyasema kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Kwekanga muda mchache baada ya kutembelea zahanati ambayo imejengwa miaka 17 iliyopita lakini haijakamilika na wananchi wanaendelea kukumbana na changamoto ya kutembea umbali mrefu kwenda kutafuta huduma za afya.
Mkuu wa Wilaya huyo alisema fedha zimeletwa ili zahanati imalizike lakini baadhi ya viongozi kwa kushirikiana na kamati ya maendeleo ya kata wakaamua kubadilisha matumizi ya fedha kwa kuzigawa kwa kila Kijiji kwaajili ya uchaguzi huo wa serikali za mitaa.
“ Wale wote walioshiriki kutoa kibari cha kubadili matumizi na kuzigawa fedha hizo za zahanati watazitapika kwani Sheria ya fedha inataka fedha inayoletwa kwaajili ya mradi itumike kweye mradi husika yaani hata kama amechaguliwa atazitapika na nitaonyesha mfano’’ Alisema Mkuu huyo wa Wilaya
Lazaro alisema kuwa yeye kazi iliyomleta ni kusimamia miradi ya maendeleo hivyo hayuko tayari kuona fedha ya serikali ikitafunwa au ukibadilishwa matumizi wakati mradi husika haujaisha nakuongeza kuwa hakuna kiongozi mkuu kwenye fedha za serikali.
Mkuu huyo wa wilaya alisema mifuko ya jimbo kwa wilaya ya lushoto haitendewi haki inahujumiwa sababu hata kule bumbuli kuna mil tano iliyokuwa imepangiwa Kwenye miradi ya maendeleo kule Kijiji cha Yamba lakini hazikutumika zikarudishwa hazina hii inasikitisha kwakweli
Alisema pia maelezo aliyopewa ya matumizi ya fedha yaliotumika kwenye zahanati hiyo mpaka sasa yanakinzana na maelezo aliyoyatoa Mbunge wa jimbo hilo Shabani Shekilindi wakati akimpa taarifa namna serkali kuu na mfuko wa jimbo na fedha binafsi zilivyotumika.
Awali akisoma taarifa Mtendaji wa Kijiji hicho mbele ya Mkuu huyo wa wilaya na mbunge ilionesha kuwa mfuko wa jimbo umechangia mil 1.4 nguvu za wananchi sh million 6 na ofisi ya Mkurugenzi iliwapatia mifuko 20 ya saruji .
Kwa upande wake Mbunge wa jimbo hilo Shabani Shekilindi maarufu kama Bosnia alisema zahanati hiyo ni kati ya zahanati ya kwanza kujengwa katika kata hiyo lakini imekuwa ya mwisho kukamilika inasikitisha kwakweli.
Mbunge huyo alisema kuwa yeye anapigana kuhakikisha wananchi wanaondokana na changamoto mbalimbali lakini wanatokea wajanja wanabadilisha matumizi , ‘’ Mkuu wa wilaya sitavumilia kuona wananchi wangu wananyanyasika naomba uchukue hatua za kisheria ili wananchi wangu wapate huduma ya afya kwa ukaribu.
“ Miaka mitano iliyopita ya ubunge wangu nilikuwa naipelekea zahanati hii fedha za mfuko wa jimbo lakini zilikuwa zinapigwa tu hata vifaa nikipeleka vinapigwa sasa kwa kuwa wewe mkuu wa wilaya ni jembe naomba uchunguze jambo hili na ulichukulie hatua kali za kisheria ili tukomeshe tabia hii sababu wananchi wanapoteza Maisha , wanajifungulia njiani kwa kukosa huduma ya afya karibu” Alisema Mbunge huyo .
Hata hivyo Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Lushoto Emanueli vuli alisema kuwa kwa mujibu wa sheria Mbunge anamamlaka ya kupeleka fedha kwenye kata na Kamati ya Maendeleo ya kata WDC pia inamamlaka yakupanga na wao ndo wanavipaumbele lakini sisi kama halmashauri tutalifanyia kazi hili.