Web

Diamond ashinda tuzo ya Msanii Bora Afrika




Msanii wa Bongofleva na Bosi wa WCB, Diamond Platnumz amefanikiwa kushinda tuzo ya Msanii Bora wa Mwaka 2021 Barani Afrika (African Artiste of The Year) kutoka Ghana Music Awards UK.



Diamond alikuwa akishindana tuzo hiyo na mastaa wengine Afrika akiwemo Burna Boy, Davido, Wizkid, Master KG, Fireboy, Mercy Chinwo, Judikay, Teni, Sinach, Patoranking.



Hafla ya ugawaji wa tuzo zimefanyika usiku wa kuamkia leo huko jijini London kwenye Ukumbi wa Royal Regency.

Staa huyo wa Bong Fleva pia yupo kwenye kinyang’anyiro cha tuzo za  All Africa Music Awards (AFRIMA) na African Muzik Magazine Awards (AFRIMMA) jina lake likiwa kwenye vipengele mbalimbali.

Kwa sasa Diamond yupo kwenye ziara yake ya muziki nchini Marekani.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad