Usiku wa Aprili 14 kuamkia 15, mwaka 1912, meli kubwa ya Titanic ilizama majini. Ilikuwa ikitoka Southampton, England kwenda New York, Marekani.
Lakini kabla ya kufika safari yake iligonga barafu gumu na kuzama katika bahari ya Atlantiki. Zaidi ya watu 1,500 walizama, ingawa watu karibu 700 walinusurika katika ajali. Na kilichowanusuru ni mawasiliano ya redio.
titanic
Nini kilitokea na kusababisha watu kuzama na kupoteza maisha?
Saa 5.40 usiku wa Aprili 14, 1912, ikiwa inakatiza katika bahari ya Atlantiki, meli hiyo iligonga mwamba wa barafu. Meli hiyo ilikatika katikati na maji yalianza kuingia ndani.
Thomas Andrews, aliyebuni michoro ya meli ya Titanic, wakati ikizama na yeye alikuwa kwenye meli hiyo.
Akatathimini athari za meli hiyo zilizosababishwa na barafu na kumwambia nahodha kwamba meli hiyo itazama.
Marconi, mfumo wa mawasiliano ya redio kwenye meli hiyo ukaanza kutuma ujumbe wa kuomba msaada kuanzia 6.15 usiku kwa kutumia mashine ya ‘telegraph’ isiyotumia waya.
Ujumbe huo unatajwa kusaidia kuokoa maisha ya watu zaidi ya 700.
Jack
Msimamizi wa mawasiliano ya redio ya meli ya Titanic, Jack Phillips alituma ujumbe katika meli za Carpathia na Frankfurt zilizokuwa katika safari kwenye bahari hiyo, kwamba meli yao imegonga barafu na inaweza kuzama.
“Tunawaweka abiria kwenye boti ndogo, wanawake na watoto, umeme utakatika wakati wowote’.
” Nyie wapumbavu. Jiandaeni. Kaeni chonjo” ulikuwa ujumbe kutoka Titanic.
”Tunazungumza kutoka Titanic. Maji yaningia kwa kasi kwenye chumba cha injini, “Jack Phillips alisema katika maelezo yake.
Jack Phillips hakupona kwenye ajali hiyo na anatajwa mara kadhaa kwenye tukio hilo kwa ujasiri na akili aliyotumia.aaa
Meli nyingine wakati huo hazikuwa zikiamini kwamba ujumbe huo ulikuwa unatoka kwenye meli ya Titanic. Umeme ulikatika mpaka kufikia saa 8.10 usiku.
Mfumo wa kutuma ujumbe wa mawasiliano wa ‘Marconi’ ukasimama kufanya kazi kwa sababu ya umeme. Sehemu ya mbele ya meli ilikua imeshazama, huku ya nyuma ikiwa juu. Dakika 10 baadaye yaani saa 8:20 usiku, meli hiyo ilikatika vipande viwili na vipande vyote vikazama.
Saa mbili baada ya kuzama, meli ya Carpathian iliwasili katika eneo la ajali. Na kwa kutumia boti za kuokoa, watu 700 waliosalia wakaokolewa.
Inakadiriwa watu zaidi ya 1500 walizama usiku ule katika bahari hiyo iliyokuwa barafu kutokana na hali ya baridi iliyokuwepo. Ujumbe wa mawasiliano kwa meli ya Carpathian ungepuuzwa pengine watu wote ama wengi zaidi ya waliokolewa wangepoteza maisha.
Jack
Nini kinafuata?
Mabaki ya meli hiyo ya Titanic yalikuja kugundulika na kuonekana mwaka 1985, kilometa 740 km mwa Newfoundland, Canada. Kampuni ya RMS Titanic iliomba kuyaondoa mabaki hayo mwaka 1980.
Tangu mwaka 1987, kampuni hiyo ilipeleka watu chini ya maji mara nane mpaka sasa kutafiti na ikagundua mabaki karibu 5,500 ya vitu mbalimbali ikiwemo sarafu za fedha na sarafu za dhahabu.
RMS Titanic pia imepanga kutumia roboti ya chini ya maji ili kusaka mfumo wa mawasiliano wa Marconi’ uliookoa mamia ya watu.