Fahamu Kuhusu Gari Aina ya Suzuki Jimny au “Wanna Be-Baby G-Wagon”


Suzuki Jimny au “wanna be-baby G-Wagon” ila kuna ka doubt kidogo kuhusu hilo jinaa 😄 lakini tuendelee

Miaka ya 1970, hili gari lilikuwa linamilikiwa na wafanyakazi level ya wakusanya kodi au wanasheria wadogo..

Kwa kuliangalia, huwezi tegemea kama lishawahi kushinda world record ya kupanda milima kwa umbali wa mita 6688 ( kuzidi hadi Kilimanjaro ).. ukiachana na hiyo, hii kuanzia generation ya 3 ndo ubora umezidi kwa hali ya juu


Hii ni moja ya crossover SUV nzuri kwenye ulaji wa mafuta na pia mfumo wa 4WD.. unlike magari mengine ya kipindi cha 2002, hili ilikuwa na vaccum-lockng hubs ambayo gari ikiwa speed ndogo (chini ya 100kph) hutumia 2WD na ikizidi 100kph ina engage AWD kwaajili ya usalama zaidi coz kama tunavo jua Gari za 4WD zinakua na traction nzuri barabarani hivyo husaidia katika kona na sehemu zenye utelezi.

Sasa, kwenye hii latest model, imekuja na mabadiliko mengi kuanzia bodyframe design, automatic brake assist, high beam assist, infotainment na kwenye engine, imewekwa kubwa ya 1.5L .. haya yotee yaliwekwa kwenye suzuki ya 2018, ila wakati zina anza tengenezwa miaka ya nyuma hawakuwa na uhakika kama watu watazipenda ila chakushangaza, demand imekuwa kubwa hadi sasa wameamua ku merge na Maruti (kampuni ya india) kutengeneza zitakazo kuja Africa na Middle east...

Amini usiamini Suzuki jimny ina itoa jasho Range rover na land cruiser offroad. Inauwezo mkubwa sana offroad na kinacho ifanya iwe bora zaidi ni kuwa na shortwheelbase hivyo kuwa na uwezo mkubwa waku jivuta hasa likiwa lime kwama mahali.

By @east_cars

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad