Mwanamitindo na mzazi mwenza wa Staa wa Bongofleva, Rayvanny, Fahyvanny amesema sababu za kutobadilisha jina analolitumia kwenye mtandao wake wa Instagram linalounganisha jina lake na Rayvanny yaani (Fahyvanny), ni kutokana jina hilo limehalalishwa na mtandao huo kwa hiyo ni ngumu kulibadilisha
“Hata kama nikibadilisha jina itakuwa haina maana yeyote kwani nitaonekana mimi nina matatizo, lakini sisi tuko poa na hatuna shida yoyote pia tuna mawasiliano mazuri kama wazazi,” amesema.
Aidha, Mwanamitindo huyo amekanusha sauti zilizozagaa mitandaoni wiki kadhaa zilizopita zikisikika kumuagiza dereva wa bodaboda amfuatilie mpenzi wa sasa wa mzazi mwenzie Rayvanny, Paula ambaye wapo kwenye mahaba mazito.
Katika hatua nyingine amesema hana matatizo na baba wa mtoto wake kwa kuwa anawahudumia vizuri yeye na mwanaye.
Ajira: 9 FORM FOUR and Above Job Opportunities at Zanzibar Beach Resort September, 2021 - Various Posts
Fahyvanny ambaye amefunguka kwa mara ya kwanza baada ya kuachana na Rayvanny, amesema anamheshimu sana msanii huyo ambaye ni CEO wa lebo ya Next Level Music (NLM).