Fei Toto Afunguka "Kwa Mwendo Huu Nitawafunga Sana Mabao ya Mbali"





KIUNGO wa Yanga, Feisal Salum ‘Fei Toto’ amewachimba mkwara makipa wa Ligi Kuu Bara kwa kusema kuwa atahakikisha anaendelea kufunga mabao ya mashuti ya mbali katika kila mchezo ambao ataweza kufanya nafasi ya kufanya hivyo.

 

Kiungo huyo ambaye kwa sasa amekuwa kwenye kiwango bora msimu huu ambapo tayari amefanikiwa kufunga mabao miwili katika michezo mitatu ya msimu huku moja akifunga nje ya eneo la 18.

 

Fei ametoa kauli hiyo kuelekea kwenye mchezo dhidi ya Azam ambao unatarajia kupigwa Oktoba 30, mwaka huu kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar ukiwa ni mchezo wa nne kwa timu hizo kwenye msimu huu.

 

Akizungumza na Championi Jumatatu, Fei alisema kuwa suala la yeye kuendelea kufunga mabao ya mbali ni mmoja ya malengo kwa kuhakikisha anafanya hivyo katika kila mchezo kutokana na nafasi atakayoweza kupata kwa malengo ya kusaidia timu yake.

 

“Suala la kufunga ni jambo muhimu kwa sababu ndiyo maana tupo kwenye ligi ambayo kila timu inahitaji kushinda ili kupata matokeo kitu ambacho tumekuwa tukipambania msimu huu na ukweli tunamshukuru Mungu tumeanz

 

“Ifahamike ligi ya msimu huu ni ngumu, kwa mechi ambazo tumecheza nimekuwa nikiliona hilo licha ya matokeo mazuri upande wetu, yale mabao ya vile nadhani nitaendelea kufunga kwa nafasi ambazo zitakuwa zinapatikana kwa sababu nataka kuisaidia timu yangu kufikia malengo,” alisema Fei Toto.

IBRAHIM MUSSA, Dar es Salaam

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad