Qatar yafanya uchaguzi wa kwanza wa bunge




Raia nchini Qatar wanafanya uchaguzi wa kwanza wa bunge katika taifa hilo la Kiarabu hii leo hatua inayoashiria demokrasia ambayo hata hivyo wachambuzi wanasema haitaathiri kwa namna yoyote mabadilishano ya kimamlaka kutoka kwenye familia ya kifalme. 


Wabunge 30 wanapigiwa kura miongoni mwa 45 wa baraza lenye ushawishi mkubwa la Shura lenye ukomo wa kimamlaka ambalo awali liliteuliwa na amiri kama baraza la ushauri.Raia walianza kupiga kura mapema hii leo na matokeo yakitarajiwa kutoka baadaye. 



Waangalizi wanasema uamuzi wa kufanya uchaguzi ambao chini ya katiba ya mwaka 2004 unatakiwa kufanyika ingawa uliahirishwa mara kadhaa kwa maslahi ya kitaifa unafanyika katikati ya uchunguzi mkali wakati Qatar ikijiandaa kuwa mwenyeji wa michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2022. 



Baraza hilo la Shura litaruhusiwa kupendekeza sheria, kuidhinisha bajeti na kuwachagua mawaziri.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad