Hanstone Kama Rich Mavoko, Wana Mkataba wa Maisha Pale WCB



Chawa Pro Max, @officialbabalevo ameleak kilicho nyuma ya zile rumors za hivi karibuni kuhusu kinachoendelea kati ya Hanstone na uongozi wa WCB. B Levo amedai ilibidi Hanstone awe ametoka mwezi wa 5 mwaka huu ila akajifelisha mwenyewe.

Kwa mujibu wa Baba Levo ni kuwa,Mwezi wa kwanza mwaka huu @diamondplatnumz alimuita Hanstone na kumwambia anamuachia mwezi Mei hivyo amletee nyimbo 5 zilizokamilika ili jambo liishe lakini cha Ajabu Tone alikuwa hana hata wimbo mmoja uliokamilika ukizingatia kakaa WCB zaidi ya mwaka, baadhi ya nyimbo zilikuwa zina verse bila Chorus na nyingine Verse moja na Chorus.

Baada ya hapo Tone akaanza kuandaa nyimbo lakini Diamond hakutoa tena tarehe ya lini msanii huyo angetoka, B levo anadai Diamond alipanga akitoka Marekani amuachie Tone kama surprise ila akakutana na EP ya jamaa imeachiwa mitandaoni.

Mkataba wa Hanstone alioingia WCB ni wa maisha sawa na ule wa Rich Mavoko, hivyo kijana atulie kama mwenzie maana hachomoki kirahisi. Hiyo ni kwa mujibu wa Chawa pro max alipokuwa Serena Hotel hii leo akiongea na waandishi wa Habari.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad