Nimewatazama Young Africans kwenye game tatu za mwanzo, Ngao dhidi ya Simba na mbili za TPL, specifically Kagera na hii Geita Gold
Ni hivi dakika 90 za mchezo zimegawanyika kila Mwalimu ana focus yake! Wengine 15 za mwanzo na wengine 30 za mwanzo katika kuamua matokeo
Hawa Yanga wamefanikiwa kitu kimoja kutokana na kikosi chao! Napenda kukiita kikosi mseto, kutokana na aina ya wachezaji walionao na Mataifa yao!
Ni sahihi kusema ni Cosmopolitan Squad! Hivyo Mwalimu anatumia ubora wa wachezaji kupata matokeo kirahisi kupitia uwezo wao wa kuusoma mchezo! INSIGHT (UFAHAMU)
Yanga wakianza game wanakupress kwenye kila eneo, wanatumia faida ya presha yenu ili wao wapate matokeo, wanajua ndani ya 30 za mwanzo wanahitaji matokeo
Wamefanikiwa hilo dhidi ya Kagera dakika ya 24, dhidi ya Simba ni dakika ya 11 na leo dhidi ya Geita ni dakika ya 16! Hii ndio plan yao muhimu sana Wananchi, baada ya hapo ni ngumu kusawazisha
Wana Khalid Aucho huyu ndio kama Server! Mkija kwa kasi yeye ndie anapooza mchezo wenu na mtacheza kwa speed ya Yanga, mkipungua kasi wao wanakuja kwa kasi! Wamefanikiwa sana eneo hili
Huyu pichani anaeingia ni Mwanangu @yusuphathuman10
Leo kaanza mechi ya kwanza kwenye TPL kwenye uzi wa Yanga, hongera Ngosha😄
@jr_farhanjr
#MOROGORO