Iran yasema Israel na Marekani huenda zilihusika na shambulio dhidi ya vituo vya gesi





Mkuu wa ulinzi wa raia nchini Iran Gholamreza Jalali amezishtumu Israel na Marekani kwa kuwa washukiwa wakuu wa shambulio la mtandao lililokatiza mauzo ya petroli kote nchini humo lakini akasema uchunguzi wa kiufundi bado unaendelezwa. 
Katika mahojiano na shirika la habari la serikali nchini humo, Jalali alisema kuwa kitaalamu bado hawawezi kubainisha hilo lakini kiuchambuzi, anaamini kuwa shambulio hilo lilifanywa na utawala wa kizayuni, Wamarekani na mawakala wao.Jalali amesema kuwa kulingana na uchunguzi uliokamilika, Iran ina hakika kwamba Marekani na Israel zilihusika na mashambulizi ya mtandao kwenye reli ya Iran mnamo mwezi Julai na bandari ya Shahid Rajaee mnamo Mei 2020. 

Miaka michache iliyopita, Iran ilisema kwamba iko katika hali ya tahadhari kuhusiana na mashambulizi ya mtandaoni huku ikiwalaumu mahasimu wake ya Marekani na Israel

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad