IS yadai kuwajibika na shambulio la bomu Uganda




Kikundi cha Islamic state (IS) kimedai kuwajibika na shambulio la bomu lililomuua takriban mtu mmoja katika mji mkuu wa Uganda Kampala Jumamosi usiku.

Kikundi hicho cha wanamgambo kiliyasema hayo katika taarifa iliyotangazwa kwenye chombo cha habari chenye uhusiano na kundi hilo jana Jumapili.

Kikudi hicho kilisema kwamba baadhi ya wajumbe wake walilipua kifaa cha vilipuzi katika kilabu ambapo "wajumbe na majasusi wa serikali ya Uganda walikuwa wamekusanyika" mjini Kampala.

Bomu hilo, lilikuwa limesheheni vyuma vyenye ncha kali, liliulenga mgahawa huo maarufu kwa uuzaji wa nyama ya nuruwe (kiti moto) uliopo viungani mwa mji mkuu, polisi walisema Jumapili.

Taarifa zilizokusanywa zinaonyesha kuwa wanaume watatu, waliojifanya kuwa ni wateja, walitembelea mgahawa huo, wakaweka mfuko wa plastiki chini ya meza na kuuacha muda mfupi baada ya kulipuka, polisi ilisema.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad