Jacqueline Mengi aruka kiunzi cha kwanza Mahakama ya Rufani


Mjane wa aliyekuwa mfanyabiashara maarufu nchini, Reginald Mengi, Jacqueline Ntuyabaliwe Mengi amevuka kihunzi cha kwanza katika mapambano ya kisheria ya mirathi baada ya Mahakama ya Rufani kutupilia mbali pingamizi dhidi ya maombi yake kuhusu wosia.

Jacqueline amefungua maombi ya mapitio ya hukumu ya Mahakama Kuu iliyotolewa Mei 18, 2021 na Jaji Yose Mlyambina iliyobatilisha wosia uliokuwa unadaiwa kuandikwa na marehemu Mengi wakati wa uhai wake, ambapo anaiomba Mahakama ya Rufani ifanye mapitio ya hukumu hiyo na hatimaye ibadilishe.

Mahakama ya Rufani katika uamuzi wake ambao Mwananchi limeona nakala yake iliyotolewa na mahakama hiyo kwa matumizi ya umma, leo Jumatano, Oktoba 13, 2021, imetupilia mbali hoja zote za pingamizi dhidi ya maombi hayo ya Jacqueline na badala yake imekubali kuyasikiliza maombi hayo.
#MwananchiUpdates  

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad