Jamaa Auliza Google Jinsi ya Kuua Mtoto Mchanga, Ampa Dawa za Kifafa ili Amuue


Kijana Jamar Bailey (21), amehukumiwa jela baada ya kuuuliza mtandao wa Google namna ya kumuua mtoto mchanga kwa vidonge na kisha kumpa dawa kwa lengo la kumuua.

Kijana huyo toka eneo la Birmingham nchini Uingereza amehukumiwa kifungo cha zaidi ya miaka ishirini na tano gerezani baada ya kukiri kutenda kosa hilo kwa kumnywesha mtoto huyo dawa zinazotumika kwa watu wenye matatizo ya moyo na kifafa ziitwazo Epilim Chrono.

Inadaiwa siku ya tukio kijana huyo alitumia simu yake ya mkononi kuuuliza mtandao wa google ni jinsi gani anaweza kumuondoa mtoto uhai na baada ya kupata majibu alichukua chupa inayotumika kuhifadhia maziwa ya mtoto huyo, kisha kuweka dawa hizo na kumnywesha.

Habari zaidi zinasema polisi waliomtia nguvuni walifanikiwa kukuta ushahidi katika simu yake na pia mabaki ya dawa hizo katika chupa ambapo yvote vimetumika kama ushahidi.

Mwendesha mashtaka Sajenti Kirsty Wilson, kutoka kitengo cha ulinzi wa umma keneo la West Midlands kulipotokea kisa hicho amesema mtoto huyo wa kike ana bahati kubwa kuendelea kuishi na kuwa wanafuraha hakupoteza maisha.

Kwa sasa mtoto huyo yuko chini ya uangalizi na ulinzi maalumu kutokana na kuandamwa na matukio yanayotishia uhai wake.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad