Jeneza la kale la kasisis wa Misri lililogunduliwa mwaka jana limewekwa katika maonyesho kwa mara ya kwanza katuka monyesho ya Dubai.
Jeneza la kasisi Psamtik lilikuwa ni miongoni mwa majeneza 27 yenye rangi ambayo hiuvi karibuni yaligunduliwa katika wilaya ya Saqqara iliyopo katika mji mkuu Cairo inayofahamika kwa kuwa eneo la makaburi ya kale ya mafarao na wafalme.
Akipewa jina bandia la dokta, Psamtik alihudumu kamamkuu wa tiba wa Tutankhamun.
Wizara ya Misri ya mambo ya kale imeelezea kupata uvumbuzi mkubwa zaidi na wa muhimu zaidi katika miaka ya hivi karibuni.
Maonyesho hayo ya Dubai ni kusanyiko kubwa zaidi la dunia kufanyika tangu mwanzoni mwa janga Covid-19 , ambapo zaidi ya nchi 190 zinaonyesha tamaduni zake na uvumvuzi kwa matumaini ya kuwavutia wawekezaji.
Huku Misri ikiwa uvumbuzi mwingi na fursa kubwa ya uwekezaji ya kuonyesha katika banda lake la maonyesho, ni jeneza ambalo limekuwa kivutio kikubwa zaidi-huku wagenei wakisubiri kwenye misururu mirefu kuweza kulitazama.
"Ni muhimu kusubiri ili kuweza kuona jeneza hili la kihistoria lililotumia maelfu ya miaka iliyopita" mtalii mmoja alisema.