Kenya na Somalia Wanasubiri Hukumu itakayotolewa juu ya mpaka wa bahari

 


Kenya imesema itapuuzia hukumu itakayotolewa leo na mahakama ya kimataifa ya haki kuhusu mzozo wa mpaka wa bahari kati ya Kenya na Somalia.

Mataifa hayo mawili yamekuwa yanadai maili 62,000 katika ujazo wa mraba ambao ni sawa na kilomita 160,000 za ujazo wa mraba wa bahari ya Hindi ambapo zinadhaniwa kuwa na utajiri wa mafuta na gesi.

Hatahivyo, jinsi mpaka wa Kenya ulivyo sasa ndivyo kenya inataka uendelee kuwa. Lakini Somalia inasisitiza kuwa bandari yake ya kusini inapaswa kuepo kusini mashariki mwa mpaka.

Mpaka huu wa Kenya ulitangazwa kuanzishwa mwaka 1979.

Mwaka 2009, mataifa mawili yalisaini makubaliano ambayo yalipitishwa na Umoja wa Mataifa ili kujadili kuhusu mipaka yao.

Mwaka 2014, Somalia iliamua kutafuta ufumbuzi wa mzozo huo katika mahakama ya kimataifa ya (International Court of Justice) iliyoko Hague.

Katika ombi lake, Somalia ilisema mazungumzo ya kidiplomasia yameshindikana na sasa mahakama "iamue uratibu sahihi wa kijiografia wa mpaka mmoja wa baharini katika Bahari ya Hindi".

Lakini hayo si yote. Somalia iliitaka mahakama ya kimataifa ICJ kutangaza kuwa “Kenya… imekiuka wajibu kimataifa wa kuheshimu haki za nchi na mahakama".

Mwaka mmoja baadae , Kenya iliweka upingamizi mahakamani juu ya kesi hiyo.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad