Kesi Mbowe na Wenzake: Mahakama Yapangua Pingamizi lao




MAHAKAMA KUU, Divisheni ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, nchini Tanzania imeyatupa mapingamizi mawili ya upande wa utetezi katika kesi inayomkabili kiongozi wa chama kikuu cha upinzani nchini humo cha Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Mapingamizi hayo yalihusu maelezo ya onyo ya mshtakiwa wa pili katika kesi hiyo ya uhujumu uchumi yenye mashtaka ya kupanga njama za ugaidi ya Adam Kasekwa, yasitumike mahakamani hapo kama sehemu ya ushahidi wa jamhuri na maelezo hayo yalitolewa baada ya Kasekwa kuteswa.

Uamuzi huo wa kesi ndogo ndani ya kesi kubwa, yametolewa leo Jumatano, tarehe 20 Oktoba 2021 na Jaji Kiongozi Mistapha Siyani.

Mbali na Mbowe na Kasekwa, watuhumiwa wengine katika kesi ya msingi ya uhujumi uchumi yenye mashtaka ya kula njama za kufanya vitendo vya ugaidi ni, Halfan Hassan Bwire na Mohammed Abdillah Ling’wenya.


Kesi hiyo ndogo ndani ya kesi ya msingi, imetokana na mapingamizi ya upande wa utetezi, dhidi ya maelezo ya onyo ya mshtakiwa wa pili, Kasekwa, yaliyowasilishwa mahakamani hapo na upande wa jamhuri kama sehemu ya ushahidi wake.


Wakitaka yasitumike kwa madai kuwa yalichukuliwa kinyume cha sheria, ikiwemo mtuhumiwa kuchukuliwa maelezo hayo nje ya muda na bila ya ridhaa yake.

Kasekwa na Ling’wenya walikamatwa tarehe 5 Agosti 2020 maeneo ya Rau Madukani, Moshi Kilimanjaro na kuhojiwa tarehe 7 Agosti mwaka jana, Kituo Kikuu cha Polisi Dar ea Salaam.

Akitoa uamuzi katika pingamizi la muda, Jaji Kiongozi Siyani amesena, kifungu cha sheria namba 50 (2) na cha 51 cha Sheya Mwenendo wa Makosa ya Jinai iliyonyiwa marekebisho 2019, kinaruhusu muda wa kumhoji mtuhumiwa kuongezwa kwa masharti maalum ikiwemo mkuu wa upelelezi kuongeza muda au kuomba kibali cha kuongeza muda huo mahakamani.

Jaji Kiongozi Siyani amesema hoja ya jamhuri kuchelewa kumhoji Kasekwa kwa sababu ya mtuhumiwa huyo kuwasaidia kumtafura mwenzao Moses Lijenge mkoani Kilimanjaro na Arusha, na kumsafirisha kutoka Moshi kuja Dar es Salaam ina mantiki.

“Ni maoni yangu kwamba kuchelewa kwa kuhojiwa au kuchukuliwa maelezo Kasekwa kulikuwa na sababu na kwamba zinafananana matakwa ya sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai ya 2019 kifungu cha 50 (2). Matakwa ya sheria hiyo muda uliotumika kumkamata na kumsafirisha kuja Dar haupaswi kuwa ndani ya saa nne ambayo yanapaswa kuhesabiwa,” amesema.


Kuhusu pingamizi la mtuhuniwa kuchukuliwa maelezo kwa vitisho, Jaji Kiongozi Siyani ushahidi wa utetezi haukuthibitisha madai hayo kwa kuwa haukupinga kitabu cha mahabusu (dentetion rejesta) iliyoletwa na jamhuri kama sehemu ya ushahidi wake, kilichoonesha kuwa mtuhumiwa alihojiwa kituo kikuu central Dar.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad