Kesi Ya Sabaya Gazeti La Mwananchi Latajwa





Kutoka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha Leo Tarehe 28.10.2021 katika mwendelezo wa kesi namba 27/2021 kesi ya Uhujumu Uchumi Jamuhuri Dhidi ya aliyekua mkuu wa wilaya  Lengai Ole Sabaya na wenzake sita.

 

Ilipotimu saa 10:30 Asubuhi kesi ilianza kusikikizwa mbele ya Hakimu mwandamizi Dkt Patricia Kisinda wakili wa serikali Afmed Mtenga alisimama mahakamani na kuieleza  mahakama kuwa Shauri limekuja kwaajili ya kusililizwa

 

Kabla ya shahidi kuendelea wakili upande wa utetezi Moses Mauna akasimama katikati ya mahakama na kuomba kusajili malalamiko yao kwa mahakama

Nakusema kuwa concerning yao ipo kwananamna ambavyo kesi hii inayoripotiwa na vyombo vya habari hasa magazeti ya mwananchi .

 

Kupitia ukrasa wao wa instergram walieleza kuwa cheti kilicholetwa na shahidi mahakamani Jana  waliandika kuwa cheti kilicho kabidhiwa mahakamani kilionyesha Sabaya na wenzake wakiwa Bank wakati sio kweli.

 

Mauna alivishukuru vyombo vingine vya habari kwa kuripoti kesi hiyo vizuri Mauna akaendelea kwa kusema kuwa hii siyo Mara ya kwanza kwa Mwananchi kusema hivyo “Alikuja meneja wa TRA Shahidi wa Pili hapa mahakamani Mwananchi  wakaandika meneja wa TRA amkana Sabaya Mahakamani kitu ambacho sio cha kweli.

 

Wanachokifany hakina effect kwetu tu kina athari kwa upande wa jamuhuri na Mahakama hukumu ikitoka watu wanaweza wakawa tayari na vitu walivyowaaminisha”

Wakili Mauna Tunaleta ombi katika mahakama hii kwa kifungu cha sheria namba 392 A cha sheria ya mwenendo wa makosa ya Jinai gazeti hilo lipatiwe Gagi Oder.

 

Mahakama yako ione vyema kuwazuia mwananchi kufanya coverage ya kesi hii Ikiwa Gazeti la Mwananchi na mitandao yake ya kijamii na redio na tv zinazoshabia na Gazeti hilo la Mwananchi na wafanyakazi wake wasiruhusiwe kufanya kazi ya kuripoti kesi hii nje na ndani ya nchi na wala kutuma habari za kesi hii katika vyombo vingine.

 

Ofmed Mtenga wakili wa serikali alisimama na kusema kuwa ombi hilo Linaathiri procedingi za kesi na kwakuwa hayo mambo yamefanyikia huko nje na hazijafanyikia hapa mahakamani kesi ikiwa inaendelea

 

“Kama walikiwa wana eligetion na mtu mwingine dhidi ya huyo mtu wangetakiwa watafute njia nyingine ya kulileta jambo hilo kwa namna nyingine na zisiwepo kabisa katika procedure za kesi hii.”Wakili Mtenga

 

Wakili Felix Kwetukia wa Upande wa Jamuhuri nae pia alieleza kuwa “Nakubaliana na wakili Mauna Aplication inaweza ikaletwa kwa mdomo au kwa kuandikwa lakini hiyo application lazima iwe imtumwa kwa mlalamikiwa na impe nafasi huyo mlalamikiwa aweze kujibu.
Na hapa mahakamani Respondent au muhusika hayupo ili ajibu tuhuma hizo na kushauri atumie njia nyingine ikiwa kufungua kesi lakini sio katika mwendelezo wa kesi hii.Wakili Felix Kwetukia

 

Wakili Mosesi Mauna akasimama tena

“Kimsingi mawakili wa Jamuhuri wamekubaliana na sisi kifungu cha 392 A  kinaruhusu Maombi ya mdomo Kama sisi tulivyofanya hapa na Mwananchi wamekuwa wakiripoti Taarifa za kesi hii kila inapotajwa hapa na Leo hawapo mahakamani sasa sijui wanaandika hizo habari wakitokea wapi
na ndomana mahakama yako iliuliza hapa Mwananchi wapo? ukaona hawapo,wangekuwepo wangejibu hizo hoja.
nashaangaa upande wa jamuhuri kutetea jambo hili sijui wanamaslahi gani nalo swala hili kwa kuwa kesi hii Kama itachafuliwa itakuwa imetuchafua wote”.Wakili Mauna

 

Wakili Kwetukia akasimama na kusema Mh Hakimu wasituwekee maneno mdomoni sisi tumesema wafate utaratibu tu . Mauna akasimama na kuendelea kwa kusema “upande wa jamuhuri hawajaeleza utaratibu huo ambao wao wanataka waufate naomba mahakama yako ipokee maombi yetu na mahakama yako itoe Meseji mahususi juu ya hili ndo hayo tu”. Mauna akakaa chini. Hakimu akaomba muda wa kwenda kuandika maamuzi ya mahakama juu ya ombi hilo.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad