Kiba Amuibua Khaligraph Mwenye Kijiji Chake Bongo




KING Kiba amekuja kivingine kwa kumshirikisha msanii wa Kenya, Khaligraph Jones kwenye albam yake mpya iitwayo Only One King.

 

Amemshikisha katika ngoma iitwayo Habipty. Hajakosea, msanii huyo anasifika kwa kuwa na uwezo mkubwa wa free style na kupanga punch line katika ngoma zake. Pia ana uwezo mzuri wa kutumia lugha ya Kiswahili na Kingereza.

 

Albam hiyo ina ngoma kali nyingi kama Tamba, Let Me, Gimme Dat na ujio wa albam hiyo ambayo imeshirikisha pia wasanii wengi wa Bongo umedhihirisha kwamba King Kiba ni Mfalme wa Muziki Bongo.

 

Msanii Khaligraph Jones tumzungumzie kwa kifupi. Kutokana na uwezo wake ameweza kutengeneza kijiji chake Bongo kwa kolabo na wasanii kadhaa kutoka Bongo na ngoma hizo kufanya vizuri.

 

Khaligraph aliwahi kutoa ngoma moja na msanii wa Bongo pale alipomshirikisha Nikki Mbishi katika ngoma yake inayokwenda kwa jina Baba Yao.

Hapa chini kuna wasanii kadhaa ambao aliwahi kufanya nao kazi huko nyuma;

 

ROSA REE

Rapa Rosa Ree wa Bongo ambaye ametamba na ngoma kama Up In the Air, Dow na nyinginezo aliweza kufanya kolabo na Khaligharaph kupitia ngoma yake ya One Time ambayo waliifanyia remix.

 

Wakati remix hiyo inatoka, Rosa Ree bado alikuwa chini ya usimamizi wa Lebo ya The Industry.

Kutokana na aina ya rap anayofanya Rosa Ree kukutana na Khaligraph katika ngoma moja vilikutana vitu viwili ambavyo vina uwiano sawa.

Remix hiyo ndiyo ilikuwa ngoma ya kwanza kwa Rosa Ree kumshirikisha msanii kutoka nje ya Bongo.

 

YOUNG KILLER

Kolabo kati ya Young Killer na Khaligraph ni moja ya project ambazo zilikuwa zikisubiriwa kwa muda Bongo na mashabiki ili imekuja kutoka bila kuwa na uzito wake ambao ulikuwa ukitarajiwa.

Sababu ni kwamba ngoma hiyo ya Shots ilivuja mtandaoni kabla ya Young Killer kuitoa rasmi.

 

CHRISTIAN BELLA

Huyu ndiye msanii mmojawapo kuachia ngoma na Khaligraph, walitoa wimbo uitwao Ollah.

Pia ndiye msanii wa kwanza ambaye anaimba kufanya hivyo, wote niliowataja kasoro Rayvanny ambaye anarap na kuimba, wanafanya muziki wa rap.

 

Christiana Bella amekuwa akishirikishwa na wasanii mbalimbali wanaofanya muziki wa rap/Hip Hop kwa Bongo, alishawahi kufanya korasi ya Ngoma ya Fid Q ya Roho na ile ya Weusi ya Nijue.

Hata hivyo, alipotaka michano katika ngoma yake ilimbidi kuvuka boda hadi Kenya kuinasa sauti ya Khalighraph.

 

CHIN BEES

Chin Bees amlishirikisha Khaligraph katika remix ya Ngoma ya Kababaye; hii ilikuwa ni remix ya pili kwa Khaligraph kufanya na msanii kutoka Bongo.

 

Khaligraph aliweza kuonesha uwezo mkubwa katika kupitia juu ya mdondo wa trap wa ngoma hiyo ambao ulifanyika Wanene Entertainment na Producer Luffa.

 

Remix ya Kababaye baada ya kutoka iliambatana na remix ya Ngoma ya Nyonga Nyanga ambayo alimshirikisha Wyre na Nazizi; wote wa Kenya ila ile ya Khaligraph ilikuwa na nguvu zaidi.

 

STEREO

Baada ya kufanya vizuri na Ngoma ya Mpe Habari ambayo alimshirikisha Rich Mavoko aliona kuna umuhimu wa ngoma hiyo kuwa na remix.

 

Stereo aliweza kuwakutanisha wasanii kutoka Bongo na nje katika remix aliyofanya. Kutoka Bongo walioshiriki ni Billnass, Stamina na Jay Moe huku kutoka nje akiwa ni Khaligraph.

 

Hii ilikuwa ni ngoma ya tatu kwa Khaligraph kushiriki remix yake baada ya One Time ya Rosa Ree na Kababaye ya Chin Bees, Mpe Harari remix ambayo ilishatoka na kutamba hewani.

 

RAYVANNY

Licha ya Rayvanny kufanya vizuri katika muziki wa kuimba pia ni mzuri katika rap.

Hii inafanya kumuona katika ngoma kadhaa za Hip Hop alishirikishwa na Fid Q katika remix ya Ngoma ya Fresh, kabla ya hapo alikuwa amesharudia ngoma ya Mr II ya Sugu.

Hivyo basi haikuwa ni mshangao pale walikutana studio na Khaligraph na kutoa ngoma ya Chalii ya Ghetto, ngoma hii ilitoka na kutamba huko nyuma.

MAKALA; ELVAN STAMBULI, DAR

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad