Kichapo Cha Simba.. Viongozi wa Timu ya Simba Wanacheza Biti Tofauti na Wachezaji




Baada ya Simba kuondoshwa kwenye michuano ya Champions League leo, nimetoka kupokea simu ya Profesa wa Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam, dakika kadhaa nyuma

Katika mazungumzo akanambia timu Inahitaji utawala bora, benchi bora (technical bench) na Miundombinu (fedha na rasilimali) vyote hivi hutengeneza timu bora

Kwenye issue ya UTAWALA, Profesa alinikumbusha kuhusu ile simu yangu ya siku kadhaa nyuma kuhusu Viongozi wa timu hii kucheza biti tofauti, hakuna wimbo mmoja unaoimbwa

Profesa akaniambia Viongozi kama hawaimbi wimbo mmoja ni nadra kufanikiwa, pale Chelsea walikuwa na utata kati ya Michael Emenalo na waandamizi wenzake, ikiashia yeye kuondoshwa ndani ya Chelsea

Profesa akaendelea kunipa mifano ya FC Barcelona, wajumbe walipishana wengine wakajiuzulu na ile dhambi ya USALITI ikaishia kumuangusha mpaka Rais Bartomeu, mpaka sasa Barca inalipa dhambi ile ya usaliti

Profesa aliongea mengi eneo hili na mengine nimeyaweka nyuma ya pazia! Tukahitimisha kuwa, wanapaswa kuimba wimbo mmoja kwa ajili ya maslahi mapana, they need to sing along

Tukaja kwenye issue ya bench la Ufundi, Profesa akaniambia kwake yeye anaona kuna shida ya muendelezo (CONTINUITY) kwa klabu ya Simba kwenye CAF CL, msimu waliofika Robo kisha uliofata wakatolewa na UD Songo, msimu jana walifika robo na msimu huu wametolewa na Galaxy

Kuna shida ya kiufundi! Profesa akaniambia ya pili ndani ya eneo hilo ni Kocha Gomes Da Rosa, hii Simba tuionayo sasa ndio Gomes halisi anaeanza project yake, Simba wawe tayari kupitia mengi kwakuwa Kocha bado anajitafuta

Kifupi Prof anasema Kocha aliishi kwenye script ya Sven na sasa anaanza kuandika script yake! Wanahitaji muda, haswa na kikosi kipya baadhi ya maeneo

Mwisho Profesa akasema kitu kuhusu Miundombinu haswa FEDHA! Ni wazi project bora inalindwa kwa pesa, ndio pesa hii ilimfanya Chama na Miquisson waondoke, Simba wanaanza upya

Prof anasema, huwezi kutawala Afrika kama huna ubavu wa kiuchumi, ukiishi kwenye misingi ya FEEDER CLUB, utajenga kisha watu wanabomoa! Ndio malipo ya Football development model

@jr_farhanjr

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad