King Kiba Hakamatiki Aisee..Album yake Kiboko ya Njia Huko Mitandaoni




ALBAM mpya ya Mfalme wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba au King Kiba iitwayo The Only One King aliyoiachia Oktoba 7, mwaka huu, haikamatiki aisee.


Hadi sasa imetazamwa na zaidi ya watu milioni 19 katika mitandao mitatu. Albam hiyo yenye ngoma 16 kali, video iliyobeba jina la Oya Oya ndiyo iliyopokelewa na watu au mashabiki wengi wa muziki duniani kote.


Mitandao ambayo imetumika kuuzia nyimbo za albam hiyo ni mitatu ambayo ni Spotify, Audimack na Boomply. Katika Mtandao wa Boomply tayari imefikisha zaidi ya wafuatiliaji milioni 11, Mtandao wa Audimack imefikisha wafuatiliaji zaidi ya milioni nane na mtandao wa Sportify umefikisha wafuatiliaji zaidi ya milioni 1.6 hadi hivi sasa.


Upokelewaji huo wa albam hiyo ni hatua nzuri kwa King Kiba kwani amepewa sifa na wasikilizaji wa ngoma zake wa rika zote kwani wamesema hakuingiza maneno yasiyo na maadili kama wanavyofanya baadhi ya wasanii wa muziki wa Bongo Fleva.


“Ngoma zake zote zina maadili hajaingiza matusi kama wanavyofanya baadhi ya wasanii wa muziki huu wa kizazi kipya,” anasema Amos Kokoro aliyejitambulisha kuwa ni mdau wa muziki huo nchini.


Kutokana na hayo ni dhahiri kwamba, King Kiba ni mfalme katika muziki wa Bongo Fleva na amedhihirisha hilo baada ya kutoa albam hii ya tatu aliyoiita Only One King na kuzinduliwa akiwa na wanamuziki wengi wakubwa katika hoteli kubwa yenye hadhi kubwa ya Serena jijini Dar.


Kabla ya albam hiyo huko nyuma alitoa albam ya kwanza ambayo ni Cinderela ya mwaka 2007 na ikafuata Ali K 4Real ilitoka mwaka 2009.

STORI; ELVAN STAMBULI, DAR

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad