Baada ya kupata chini ya asilimia 52 ya kura katika uchaguzi wa urais wa Jumapili nchini Cape Verde, mgombea wa upinzani Jose Maria Neves amejitangaza mshindi .
Matokeo ya awali ambayo yametangazwa kutoka asilimia 99.4 ya vituo vya kupiga kura pia zilionesha hasimu wake mkuu, Carlos Alberta Veiga, amepata 42% ya kura.
Bwana Veiga alikua mgombe wa chama cha rais anayeondoka was thetJorge Carlos Fonseca.
Alikubali kushindwa katika mkutano na waandishi wa habari na kumpongeza Bw. Neves.
Bw. Neves, 61, aliwai kuwa waziri mkuu kuanzia 2001 hadi 2016. Alikuwa mgombe wa cha kikubwa cha siasa cha African Party for the Independence of Cabo Verde (PAICV) nchini Cape Verde.
Wakati wa kampeni alisema kuwa akichaguliwa, atashughulikia mgawanyiko unaoshuhudiwa nchini, kufufua uchumi na kusuluhisha mzozo wa afya ulisababishwa na janga la coronavirus.
Katika hotuba yake ya kwanza rasmi baada ya uchaguzi, alisema atakuwa "rais wa raia wote wa Cape Verde".
Aliambia BBC kwamba "amefurahishwa sana na ushindi wake".
Wagomba saba walishiriki uchaguzi huo wa urais. Mshindi alihitajika kupata zaidi ya asilimia 50 ya kura zilizopigwa ili kuepuka duru ya pili ya uchaguzi. Matokeo ya awali ya uchaguzi yanastahili kuidhinishwa na Tume ya Uchaguzi katika siku chache zijazo.