Download our blog’s APP from Google Playstore using the link here>>>
Sote tunajua katika ukanda wa Afrika, Nchi yetu ndio ilikuwa na mabando ya bei rahisi kuliko nchi yoyote hapa afrika (sub saharan)
Hii iligeuka kuwa silaha kwa tasnia yetu ya muziki wa bongo flava katika sura ya bara la Afrika, Ilikuwa rahisi sana msaga sumu kupata views milioni kuliko msanii wa Afrika kusini, kenya, Ghana, Zambia, n.k kupata hata robo ya hizo views.
Views zilikuwa ni silaha yetu, ziifanya hata watu wa mataifa mengine kuanza kutufatilia,
hata kwenye tuzo za kimataifa hizo views zilikuwa na uzito wake.
Ukija pia kwenye platform za kuskiliza miziki kupitia Boomplay na audiomac nako pia tulikuwa tunakmbiza maana internet ilikuwa bei rahisi.
Ila sasa tangu wikki iliyopita kiukeweli kumekuwa na mabadiliko sana huko youtube
Tukianza na youtube, hali ni mbaya, HataLavalava aliekuwa havumi sana ilikuwa kawaida kupata views laki 4 ndani ya siku lakini hadi sasa ana views kupata views 174K na hizi huenda nyingi ni za mashabiki namba 2 wa bono flava kutoka Kenya
Maua sama nae ngoma yake ipo trending number 1, tulizoea ngoma kishika usukani basi kwenye siku ya 4 itakuwa na views walaki laki 7 ila hadi sasa ni views laki 2 tu nazo si ajabu zikiwa nyingi kutoka kenya
Malkia zuchu nae naona upepo umemwendea ndivyo sivyo, video ina wiki ila ni views laki 7 tu, kiukweli zuchu ilibidi hapa awe na views hata milioni na laki 7, hapa napo wakenya wamehusika sana.
Kiufupi tutarajie anguko, Mabando kwa sasa mtu anaingia youtube kwa machale sana, i heri aingiziwe video kwenye simu yake huko vibandani.
Kwa kipindi hiki mashabiki wa kenya huenda watajaza views zaidi kuliko watanzania
Kwa sasa nadhani wa nigeria wamefurahia sana hili swala.
Huenda kabla mwaka haujaisha mabando yatapandishwa tena na huu utakuwa msumari wamoto kwenye upande wa youtube views.