ALIYEKUWA kocha mkuu wa Simba, Didie Gomes amesema ameomba kujiondoa kwenye klabu hiyo baada ya kushindwa kufikia malengo kwenye Mashindano ya Klabu Bingwa Afrika.
ALIYEKUWA kocha mkuu wa Simba, Didie Gomes amesema ameomba kujiondoa kwenye klabu hiyo baada ya kushinfwa kufikia malengo kwenye Mashindano ya Klabu Bingwa Afrika.
Gomes amefunguka hayo muda mchache baada ya uongozi wa klabu hiyo kutoa taarifa ya kuridhia ombi lake la kuachana.
Amesema anamini ni muda sahihi wa yeye kuondoka kwenye nafasi hiyo kutokana na kushindwa kufikia mafanikio.
“Malengo ya klabu yalikuwa ni kufika robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika lakini tumeshindwa kufikia hatua hiyo nimeamua kukaa kando ili kupisha wengine waweze kuifikisha timu
“Kuachana na Simba naamini ni muda sahihi amechukua uamuzi huo kutokana na kushindwa kufikia mafanikio na malengo ya klabu,” anasema.
“Nimeumia sana kushindwa kufikia malengo. Naipenda Simba naiombea ifike mbali kwenye mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika,” anasema.