Kocha Mexime aunga mkono kauli ya Kim Poulsen





Kocha wa zamani wa zamani wa Mtibwa na Kagera Sugar, Mecky Mexime ameunga mkono kauli ya kocha wa Taifa Stars, Kim Poulsen ambaye alisema kuwa kitendo cha vilabu vikongwe nchini kuwasajili wachezaji aliowajumuisha katika kikosi chake kisha kutowatumia kunamuathiri katika ujenzi wa timu imara.
Poulsen aliyasema hayo wiki moja iliyopita wakati alipotangaza kikosi kitakachoingia kambini Oktoba 3 ,2021 kwa ajili ya kujiwinda na mechi za kufuzu fainali za kombe la Dunia zitakazofanyika nchini Qatar, 2022 dhidi ya Benin ambapo amesema anapata wakati mgumu kuwajumuisha wachezaji ambao hawapati muda wa kucheza katika vilabu vyao.

Maoni ya Mexime amesema kuwa ni kweli ni ngumu kuwaita wachezaji wasiopata muda wa kucheza katika vilabu hivyo ingawa walikuwa na namba katika kikosi cha Stars, lakini hilo ni jukumu la wachezaji wenyewe ambalo ni kujituma ili watengeneze ushawishi kwa makocha wa vilabu hivyo ili wawape nafasi.

Mexime ameongeza kuwa, vilabu vinahitaji matokeo, na ili wayapate ni lazima wacheze wachezaji ambao wanajituma zaidi.

Vilevile ameongeza kuwa ni ngumu kumzuia mchezaji kujiunga na vilabu vya Simba, Yanga au Azam kwakuwa vinalipa maslahi mazuri hivyo ni suala la kuwaandaa wachezaji katika kukabiliana na ushindani katika vilabu husika.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad