NASREDDINE Nabi, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa ushindi walioupata mbele ya Geita Gold ni furaha kwao na pongezi kubwa kwa wachezaji kwa kuwa walifanya kazi kubwa kutimiza majukumu yao.
Oktoba 2, Yanga ilishinda bao 1-0 dhidi ya Geita Gold katika mchezo wa ligi uliochezwa Uwanja wa Mkapa na bao hilo lilipachikwa kipindi cha kwanza.
Ni bao la Jesus Moloko dakika ya 16 kwa pasi ya Yacouba Songne lilitosha kuipa pointi tatu Yanga ambayo imeanza msimu wa 2021/22 kwa kasi.
Mchezo wake wa kwanza Yanga ilikuwa ugenini na ilishinda kwa bao 1-0 dhidi ya Kagera Sugar pale Uwanja wa Kaitaba hivyo kwenye mechi mbili imekusanya mabao mawili ikiwa na pointi zake sita kibindoni.
Nabi amesema:"Wachezaji walijituma kusaka ushindi na kwa ambacho tumekipata wanastahili pongezi bado ligi inaanza mazuri yanakuja kwa kuwa wachezaji wanahitaji ushindi kwenye mechi ambazo wanacheza.
"Ukweli ni kwamba wamekuwa wakifanya kile ambacho tunahitaji na kunamakosa ambayo yanafanyika hilo lipo wazi lazima tutayafanyia kazi ili kuweza kuwa imara zaidi kwa kuwa bado kuna mechi zinakuja na kuna muda wa maandalizi pia," .